BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SPORT CLUB YAFUTWA SHARUBU NA MBEYA CITY KATIKA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA, AMIS TAMBWE AOKOA JAHAZI LISIZAME.



https://fbexternal-a.akamaihd.net/safe_image.php?d=AQBcMz9Flud5S4lC&w=398&h=208&url=https%3A%2F%2Ffbcdn-sphotos-h-a.akamaihd.net%2Fhphotos-ak-ash3%2Ft1%2F1932323_10202339738867600_1436879306_n.jpg&cfs=1 
Mbeya,Tanzania
WAKICHEZA soka maridadi katika kipindi cha kwanza, Klabu ya Mbeya City imefanikiwa kipata bao la kuongoza dhidi ya Klabu ya Simba, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ukiwa umepambwa na jezi za rangi za zambarau na nyeupe, imeifanya timu hiyo kung'ara katika mechi hiyo.




Mbeya City inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, iliingia uwanjani ikiwa na rekodi ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wakata miwa wa Morogoro Mtibwa Sugar.

Wakati Simba ikisafiri kutoka mjini Tanga walipochapwa na Mgambo JKT kwa bao 1-0, endapo matokeo yatabaki hivi Mbeya City itapanda mpaka nafasi ya pili ikiwa nyumba ya Azam kwa pointi moja.

Mbeya City ambayo imeingia katika Ligi Kuu kwa mara ya kwanza na kuwa tishio kwa timu za Ligi Kuu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusakata soka,kiasi cha kuongeza upinzani katika Ligi Kuu ambayo awali ilikua ikiongozwa na timu kongwe za Simba,Yanga na matajiri wa Dar es Salaam, Azam.

Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi na dakika ya 50 Aamis Tabwe akaipatia Simba bao la kusawazisha,kufutia kazi nzuri ilifanywa na Haruna Chanongo,bao la Mbeya City ilifungwa kwa njia ya penalti. chanzo http://www.habarimpya.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: