
TIMU ya JKT Ruvu leo imekuwa tishio mbele ya Klabu ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, goli la dakika 14 katika kipindi cha kwanza iliyofungwa Hussein Bunu ilitosha kuipa Maafande wa JKT Ruvu kuwa tishio mbele ya vijana wa msimbazi kwa dakika 45 za kwanza.
Katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,hata hivyo JKT Ruvu ilishindwa kutumia uzembe wa mabeki wa Simba huku mshambuliaji wake Idd Mbaga akikosa mabao ya wazi.
Dakika ya 45 Emmanuel Swita aliipatia JKT Ruvu bao 2 kwa njia ya penalt baada ya mabeki wa Simba kumchezea rafu mshambuliaji Amos Mgissa katika eneo la hatari.
Mpaka Dakika 45 za kwanza zinamalizika Simba 0 JKT Ruvu 2.
Kipindi cha pili Simba wamefanikiwa kugomboa mabao mawili huku JKT RUVU wakiongeza bao lingine na kufanya mchezo huo unaendelea kuwa Simba 2 na JKT RUVU 3. ENDELEA KUFUATILIA MATOKEAA HAYO HAPA.
0 comments:
Post a Comment