NA MTANDA BLOG, MOROGORO.
WAMILIKI
wa daladala Manispaa ya Morogoro wamekubaliana na serikali kusitisha
mgomo baada ya madai yao manne waliyokuwa wametaka
yatekelezwa,kukubaliana moja wakati wakazi wa Manispaa hiyo wakikumbwa
na adha ya kukosa usafiri kwa masaa tisa juzi mkoani hapa.
Akizungumza
na mwandishi wa gazeti hili mkoani hapa Mkuu wa wilaya ya Morogoro,
Saidi Amanzi alisema kuwa wamiliki wa daladala wamekubaliana na serikali
kurejesha huduma ya usafiri baada ya mgomo uliodumu kwa masaa tisa huku
madai mengine wakiendela kufanyia kazi.
Amanzi
alisema kuwa mgomo huo ulitokana na madai ya madereva wa daladala
kuilalamikia idara ya askari wa usalama barabarani kwa madai kuwatozwa
faini kubwa ndani ya wiki mara mbili ama tatu pindi wanapokamatwa makosa
mbalimbali.
“Jana
(juzi) madereva wa daladala Manispaa ya Morogoro walifanya mgomo wa
kutoingiza magari barabarani kwa madai kuwa wamekuwa wakitozwa faini
kiasi cha sh30,000 hadi sh120,000 kutokana na makosa mbalimbali na
askari wa kitengo cha usalama barabara lakini hoja zao tumesikiliza na
tumeafikiana baadhi zinafanyiwa kazi na nyingine wao wajirekebishe
”alisema Amanzi.
Amanzi
alisema kuwa moja ya makubaliano hayo kuondoa msongamano unaotokana na
wingi wa daladala ambayo serikali itafanyia kazi na kumepatikana eneo
lingine la stendi ambalo liko Kaloleni kata ya mjimpya.
Aidha
mkuu huyo alisema atawaeleza askari wa usalama barabarani kutumia
busara katika ukamataji unaotokana na kuegesha vibaya kutokana na stendi
hiyo kuwa ndogo.
Madai
mengine yaliyoongelewa katika kikao na viongozi wa chama cha madereva
wa daladala na wamikili sambamba na kamati ya ulinzi na usalama ni
kuwataka wamiliki kutengeneza magari yao mara kwa mara ili kuondokana na
adha ya kukamatwa na askari kwani kazi yao ni kushughulikia usalama wa
magari.
“Tumewaeleza
wamiliki na madereva baadhi ya hoja zao tutazishughulikia lakini na wao
ni lazima watengeneze daladala zao kwani kama gari ni bovu lazima
askari atalikama,na hiyo ni kazi yao na ipo kisheria,”na madai
wanayosema kuwa askari wamekuwa wakiwatolea maneno ya vitisho pindi
wanapowakamata hilo kamati yake inafanya uchunguzi kubainiki ukweli
huo,”alisema Amanzi.
Gazeti
hili lilifanya juhudi za kumfutatu Mwenyekiti wa chama cha madereva
Morogoro, Michael Mongi alisema kuwa wamekubaliana na majibu ya serikali
juu ya madai yao ya kunyanyaswa na askari wa usalama barabarani kwamba
hayatajitokeza tena.
Kulipishwa
faini kubwa, dereva kusokwa rumande, kutishiwa kwenda mahakamani na
kutukanwa na kitendo cha haki ya kusikilizwa na uongozi wa askari wa
usalama barabara na endapo makubaliano hayo hayatekelezwa madereva hao
watarejesha magari kwa wamiliki wa magari hayo.
Huduma
ya usafirishaji wa abiria ilianza majira ya saa 8 mchana huku gari aina
ya noah stendi ya daladala yaendayo nje ya Manispaa ya Morogoro na
pickup stendi ya Masika zikiendelea kubeba abiria na kutoza nauli ya sh
500 kufuatia baadhi ya daladala kufanya kazi.
0 comments:
Post a Comment