Mkuu
wa Usalama barabarani kituo cha Chalinze, Innocent Sulle akizungumza na mmoja wa majeruhi wa lori.
PICHA/MTANDA BLOG
Na MTANDA BLOG.
DEREVA wa lori la mafuta, Ally Hassan Ngoma (62)
mkazi wa Korogwe amefariki dunia papo hapo baada ya kutokea ajali iliyohusisha
gari tatu ikiwemo basi ndogo, lori na basi kubwa kugongana uso kwa uso na kusababisha kifo cha
mtu mmoja na majeruhi 38 katika ajali iliyotokea eneo la Bwawani majira ya saa
4:30 asubuhi jana mkoani Pwani.
Akizungumza na mwandishi katika eneo la tukio Mkuu
wa Usalama barabarani kituo cha Chalinze, Innocent Sulle alisema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni mwendo kasi iliyochangiwa na utelezi na ukungu iliyopelekea magari
matatu kupata ajali ikihusisha basi ndogo la abiria la Linowele Classic, lori la
mafuta na basi la Adventure na kusababisha kifo cha mtu mmoja na marejeruhi 38.
Sulle alitaja magari hayo kuwani basi la Adventure
lenye namba ya usajili T335 CCD, basi ndogo aina ya Tata T252 CHN na lori la
mafuta Iveco T613 ADH ajali ambayo ilitokea majira ya saa 4:30 asubuhi na kusababisha foleni
takribani saa moja na magari mengine kushindwa kupita kutokana na ajali hizo.
“Hii ajali imetokea majira ya saa 4:30 asuhuhi eneo
hili la Bwawani shule ya sekondari Bwawani na kusababisha kifo cha dereva wa
lori la tanki la mafuta baada ya kugongana uso kwa suo na basi ndogo aina ya
Tata na majeruhi 38 walikimbizwa zahanati ya shule ya sekondari Bwawani”.
Mkuu huyo ambaye ni Mkaguzi wa Msaidizi wa Polisi
alisema kuwa lori la mafuta lilikuwa likitokea Mwanza kueleka Dar es Salaam
lakini lilipofika eneo hilo la shule ya sekondari Bwawani iligongana uso kwa
uso na basi ndogo la abiria aina ya Tata iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam
kueleka Malinyi mkoani Morogoro wakati ikijaribu kulipita gari nyingine eneo hilo.
Sulle alisema kuwa basi la Adventure Nissan Diesel
lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Musoma lilipata ajali wakati
likikwepa kugongana na magari hayo ambayo yalikuwa barabarani na kukita katika mfereji na kuegemea upande mmoja wa mlango wa abiria.
Naye Mganga Mkuu wa zahanati ya shule yasekondari
Bwawani mkoani Pwani, Razal Mdeka
alisema kuwa majira ya saa 4:30 asubuhi alipokea majeruhi 38 kati ya hao 24
walitibiwa na kuruhusi huku 14 wakiwa na hali mbaya ambao walikimbizwa katika
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Mdeka alisema kuwa majeruhi hao waliumia sehemu
mbalimbali za miili yao ikiwemo kuvunjika miguu, mikono na viungo vingine na
jopo la madaktari kutoka kituo cha afya Magereza Bwawani waliweza kushikiana
vema kutoa huduma kwa majeruhi hao.
“Kuna majeruhi 14 wao hao zao sio mzuri na baada ya
kuona hivyo tulichukua jukumu la kuwakimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Morogoro ambayo ndiyo ipo karibu lakini hao majeruhi idadi yao ilikuwa 38 ”.
alisema Mdeka.
Mmoja wa abiria wa basi ndogo la aina ya Tata,
Gervas Kisewime (57) alisema kuwa ajali hiyo ilitokea wakati dereva wao
aliyetambulika kwa jina moja tu la Mussa kutaka kulipita lori na kujikuta
wakigongana uso kwa uso na lori la mafuta lililokuwa likitokea Morogoro kueleka
Dar es Salaam.
“Kulikuwa na mvua inanyesha, ukungu na barabara
lazima iwe itateleza hivyo vyote vimetokea katika ajali yetu hata lile basi la
Adventure nalo lilipata ajali kwa sababu ya utelezi”. Alisema Kisewime.
Ajali hizo zilizohusisha magari matatu eneo hilo la
Bwawani katika barabara kuu Morogoro-Pwani zilisababisha kuwa na foleni kubwa
kwa pande zote mbili kwa mabasi ya abiria kukwama kwa saa moja kutokana na basi
ndogo kuziba barabara ambapo kikosi cha askari wa usalama barabarani
walifanikiwa kutatua kero hiyo.
0 comments:
Post a Comment