Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi.
ANATUMIA fursa hii kukutana na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya kutoka Vyombo mbalimbali wa Habari ikiwa ni nafasi ya kutoa tathmini ya Hali ya Uhalifu kwa Mkoa wa Mbeya pia kusikia maoni, ushauri na changamoto mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari kwa lengo la kujenga na kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
TATHIMINI YA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA FEB.
2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN- 2014.
1. TATHMINI YA MAKOSA YOTE YA JINAI.
Katika kipindi hicho cha Feb –2014 jumla ya makosa 2,003 yaliripotiwa, wakati kipindi kama hicho mwezi Jan – 2014 makosa 2,438 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 435 sawa na asilimia 18.
2. TATHMINI YA MAKOSA MAKUBWA YA JINAI.
Katika kipindi hicho cha Feb – 2014 jumla ya makosa makubwa 196 yaliripotiwa, wakati kipindi cha mwezi Jan-2014 makosa 212 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 16 sawa na asilimia 8.
3. TATHMINI YA MAKOSA YATOKANAYO YA JITIHADA ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA WADAU WENGINE.
Aidha katika kipindi cha Feb – 2014 makosa makubwa yatokanayo na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali katika kufanya doria, misako na operesheni katika kupambana na uhalifu na wahalifu yaliripotiwa matukio 40, wakati kipindi mwezi Jan- 2014 yaliripotiwa makosa 56, hivyo kuna pungufu ya matukio 16, sawa na asilimia 29.
4. TATHMINI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
Kwa upande wa maosa ya usalama barabarani jumla ya makosa/matukio yote yaliyoripotiwa katika kipindi cha Feb – 2014 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishaji ni 3,817 wakati kipindi mwezi Jan- 2014 yaliripotiwa makosa 4,416 hivyo kuna pungufu ya makosa 599 sawa na asilimia 14.
Matukio ya ajali yaliyoripotiwa kwa kipindi cha Feb – 2014 yalikuwa 29 wakati kipindi cha Jan- 2014 yalikuwa 38 hivyo kuna upungufu wa matukio 9 sawa na asilimia 24.
Matukio ya ajali za vifo yaliyoripotiwa Feb – 2014 yalikuwa 15 wakati kipindi cha Jan-2014 yaliripotiwa matukio 27 hivyo kuna pungufu ya matukio 12 sawa na asilimia 44.
Watu waliokufa kipindi cha Feb- 2014 walikuwa 18 wakati Jan -2014 walikuwa 30 hivyo kuna pungufu ya watu 12, sawa na asilimia 40. Watu waliojeruhiwa kipindi cha Feb – 2014 walikuwa watu 22 wakati Jan – 2014 walikuwa watu 49 hivyo kuna pungufu ya watu 27 sawa na asilimia 55.
Katika kipindi cha Feb – 2014 jumla ya makosa 3,788 ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo la Tshs 100,920,000/= ikilinganishwa na tozo la Tshs 131,340,000/= iliyokusanywa katika kipindi Jan – 2014 kutokana na makosa 4,378, hivyo kuna pungufu la kiasi cha tshs 30,420,000/= sawa na asilimia 23.
5. MAJEDWALI KUONYESHA HALI YA UHALIFU.
MCHANGANUO WA MAKOSA YOTE MAKUBWA YA JINAI NA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI CHA FEB – 2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JANUARI, 2014.
MAKOSA
FEB– 2014
JAN – 2014 TOFAUTI +/- ASILIMIA %.
MAKOSA DHIDI YA BINADAMU
MAUAJI
17
22
-5
-23
KUBAKA
36
44
-8
-18
KULAWITI
5
6
-1
-17
KUTUPA MTOTO
-
1
-1
-100
USAFIRISHAJI BINADAMU
3
-
+3
+300
JUMLA
61
73
-12
-16
MAKOSA DHIDI YA KUWANIA MALI
UNYANG’ANYI WA K/SILAHA
1
2
-1
-50
UNYANG’ANYI WA K/NGUVU
13
9
+4
+44
UVUNJAJI
36
26
+10
+38
WIZI
291
440
-149
-34
WIZI WA PIKIPIKI
11
20
-9
-45
WIZI WA MIFUGO
18
15
+3
+20
JUMLA
370
512
-142
-28
MAKOSA DHIDI YA MAADILI YA JAMII
(YATOKANAYO NA JITIHADA ZA POLISI KWA USHIRIKIANO NA WADAU NA WANANCHI MBALIMBALI)
KUPATIKANA NA SILAHA
2
2
-
-
BHANGI
18
26
-8
-31
NYARA ZA SERIKALI
-
3
-3
-300
POMBE YA MOSHI.
17
15
+2
+13
WAHAMIAJI HARAMU
3
-
+3
+300
JUMLA
40
46
-6
-13
0.
MATUKIO YA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI FEB - 2014 NA JAN 2014
MATUKIO
3,817
4,416
-599
-14
MATUKIO YA AJALI
29
38
-9
-24
AJALI ZA VIFO
15
27
-12
-44
WALIOKUFA
18
30
-12
-40
WALIOJERUHIWA.
22
49
-27
-55
AJALI ZA MAJERUHI
14
11
+3
+27
MAKOSA YA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI
3,788
4,378
-590
-14
TOZO [NOTIFICATION]
100,920,000/=
131,340,000/=
-30,420,000/=
-23.
WITO WA KAMANDA:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati za wahalifu na uhalifu katika maeneo mbalimbali ikiwa ni kwa ya ujumbe mfupi wa maneno, mazungumzo ya simu au kwa kufika moja kwa moja kituo cha Polisi.
Halikadhalika Jeshi la Polisi katika kuhakikisha linafanya kazi kwa karibu zaidi na wananchi, tumeunda Vikosi Kazi [Task Forces] kwa ngazi ya Kata na Tarafa. Kwa takwimu za sasa, Mkoa wa Mbeya una jumla ya Kata 218 na Tarafa 27.
Kwa Kuzingatia Weledi katika kutoa huduma bora kwa Wananchi, Jeshi la Polisi, limeweka Askari Kata katika kila Kata ambaye anashilikiana kwa karibu zaidi na wananchi na Uongozi wa Serikali ya Mtaa/Kijiji katika utoaji wa huduma. Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi kwa sasa lina Mkaguzi wa Tarafa katika kila Tarafa ambaye anafanya kazi na kikosi chenye jumla ya askari wasaidizi wapatao 15.
Lengo la Jeshi la Polisi ni kuimarisha ulinzi na usalama na kuhakikisha linafanya kazi na Wananchi kwa karibu zaidi ikiwa ni pamoja na kutambua maeneo yenye wahalifu/uhalifu na kuyashughulikia kwa haraka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya pia anatoa shukrani kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya kwa ushirikiano mkubwa wanaoonyesha kwa Jeshi la Polisi na kwa wananchi kwa njia ya kuhabarisha umma.
Aidha anatoa wito kwa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi yao ya uandishi wa habari [media ethics] ili kuepuka kupotosha umma na kuleta machafuko nchini.
“Ni imani yetu kuwa vyombo vya habari vinapotumika vizuri yaani kwa kufuata na kuzingatia maadili ya kazi ni matumaini yetu uleta mabadiliko na maendeleo kwa jamii husika, ni wajibu wetu kufikisha ujumbe sahihi na kwa wakati, ni wakati wa kuandaa vipindi vya kuelimisha jamii (educative programmes), vipindi vya kuhabarisha (informative programmes), vipindi vya kuhabarisha na kuburudisha (infortainment programmes) kwa lengo la kujenga misingi mizuri na imara zaidi kwa jamii kwa ujumla hasa vijana na watoto.
Rai yangu kwa wamiliki wa vyombo vya habari kujijengea tabia ya kufanya tathmini ya utendaji wao ikiwa ni pamoja na kukusanya maoni kutoa kwa wasikilizaji.
Pia ni vyema kufanya jitihada za dhati kutanua usikivu wa matangazo ya vyombo vya habari [media coverage) kwani kuna wananchi wengi wenye mahitaji ya kupata matangazo sambamba na kupata elimu kupitia vyombo vya habari.
Imetolewa na:
AHMED Z. MSANGI – SACP.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / HII NI TAARIFA YA MKUTANO WA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NA VYOMBO VYA HABARI, JESHI LA POLISI LASHIRIKIANA VYEMA NA WANANCHI KATIKA KUFICHUA WAHALIFU, MATUKIO 96 YALIPOTIWA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment