MAGU.
HEBU fikiri... Unaamka asubuhi na kukuta kundi la majirani nje ya mlango wa nyumba yako. Uwepo wao siyo kwa lengo la kukusalimu, bali kukupa ujumbe wa hatima ya maisha yako.
HEBU fikiri... Unaamka asubuhi na kukuta kundi la majirani nje ya mlango wa nyumba yako. Uwepo wao siyo kwa lengo la kukusalimu, bali kukupa ujumbe wa hatima ya maisha yako.
Hali hii ndiyo iliyomkuta Veronica Kibuga (85)
mkazi wa Kitongoji cha Kahangala wilayani Magu, Mwanza ambaye kwa miezi
kadhaa amekuwa akiishi kwa hofu kwani anasubiri utekelezaji wa ‘adhabu
ya kifo’ kukatwa kwa mapanga kutokana na tuhuma kuwa yeye ni mchawi.
Ujumbe uliotumwa kwake uliandikwa kwa lugha ya Kisukuma na
ulikutwa kisimani ambako waliupeleka walipokwenda kuteka maji na
unasema: “Bamayo yashikaga izamu igawo ya kukatwa mapanga”, ukimaanisha:
‘Imefika zamu yako ya kukatwa mapanga’.
Majirani wamejaa nje ya nyumba ya Kibuga kwani
wanafahamu fika kwamba mwandishi wa ujumbe ule hatanii, kwani wote
waliowahi kupata ujumbe kama wake waliuawa. Huyu ni mmoja, lakini ukweli
ni kwamba wanawake wengi, hasa wazee wanaishi na makovu na wengine
wamepoteza maisha baada ya kupokea taarifa kama hizi.
Wakati dunia nzima ikisherekea Siku ya Mwanamke
Duniani leo hii, wanawake wa aina ya Kibuga wako ndani wamejifungia
wakihofu usalama wao kutokana na kuishi katika jamii ambayo inamwona
kama mkosi na chanzo cha matatizo yote.
Wanawake wanasherehekea leo na kutukuzwa kwa
mchango wao mkubwa katika masuala mbalimbali, lakini wapo wanaohitaji
ukombozi ili watoke kwenye madhila ambayo yamewafanya kuishi kwa
wasiwasi mkubwa.
Hata watoto wadogo wanapofariki, huwa inaaminika
kuwa mwanamke mchawi ndiye ‘aliyemla nyama’. Dhana hii imewafanya baadhi
ya wanaume vijijini kuwaachia wanawake kazi ya kuchimba makaburi.
Haya ndiyo yaliyomkuta Kibuga ambaye leo hii anatembea na waraka wa kifo mkononi, akisubiri ‘siku ya hukumu yake’.
Simulizi yake
Kabugu anasema: “Siku moja niliamka asubuhi na
kukuta majirani zangu wakiwa nje ya nyumba yangu, walikuwa wameniletea
ujumbe wa kifo kutoka kwa mtu asiyejulikana akisema ataniua mimi na
watoto wangu kwa kuwa ni wachawi.”
Barua hiyo iliyotumwa na mtu anayejiita ‘Meneja wa
Kujiajiri’ ilieleza kuwa Januari 30 atafika katika nyumba ya bibi huyo
na kummaliza kwa kumkata mapanga yeye na familia yake.
Watoto wa Veronica ambao ni Usia na Magdalena
Kibuga nao wametajwa kuwa watauawa pamoja na mama yao kwa kuwa
wanasaidiana naye katika masuala ya uchawi.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment