BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KURA ZA SIRI NA WAZI BADO NI MFUPA UNAELEKEA KUSHINDIKANA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA ?.


Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila akimlalamikia Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo kwa kutompa nafasi ya kuchangia bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Silvan Kiwale.

DODOMA.

WAKATI wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakipitisha Rasimu ya Kanuni za kuendesha Bunge hilo, suala la aina ya kura kwa ajili ya kuamua masuala mbalimbali, limekwama na litaamuliwa na wabunge baada ya kuanza kwa vikao rasmi vya Bunge hilo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa mvutano wa takriban wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38 kinachoeleza aina ya kura kati ya wazi na ya siri.


Hata hivyo, wajumbe wawili wa Bunge hilo, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Felix Mkosamali wa NCCR- Mageuzi walisusia kupitisha azimio la kukubali Kanuni za Bunge hilo, wakidai kusalitiwa katika uamuzi huo na wenzao walioko kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).


Wajumbe na viongozi mbalimbali wa vyama vyenye ushawishi bungeni, kwa pamoja waliridhia na kulegeza misimamo yao ili upatikane mwafaka wa kutengeneza Katiba Mpya ndani ya wakati.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti ndani na nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, viongozi hao walisema masilahi ya Watanzania katika mchakato wa Katiba ni ya muhimu kuliko masilahi binafsi ya makundi.


Kinana asema Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahaman Kinana alisema pamoja na malumbano makali yanayoendelea katika Bunge la Katiba, anaamini sasa Katiba itapatikana.


Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana mjini Dodoma, Kinana alisema haoni tatizo katika malumbano hayo na kwamba anaamini yanatokana na mitazamo tofauti ya makundi wanayotoka wajumbe.


“Pale kila kundi lina msimamo wake, iwe Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, CCM na hata makundi katika kundi la wateule wa Rais. Ilikuwa ni lazima kushuhudia mivutano ya aina hiyo,” alisema Kinana na kuendelea: “Lakini mwisho wa yote, nawaasa wajumbe kuwa na moyo wa kuvumiliana kwa sababu lazima kila kundi litetee hoja zake kulingana na tathmini yake juu ya mwenendo wa siasa na matarajio yake ya baadaye.”


Alisema kwa msingi huo, haoni tatizo kwa CCM kuweka misimamo katika baadhi ya hoja, ingawa chama hicho pia hakitasita kulinganisha nguvu ya hoja zake na hoja za wengine.


Mtikila, Mkosamali wasusia
Mchungaji Christopher Mtikila na Felix Mkosamali ndiyo wajumbe pekee waliosusia kupitisha azimio la kukubali kanuni za Bunge hilo, wakidai kusalitiwa na wenzao walioko kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).MWANANCHI

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: