MALORI 28 NA ABIRIA ZAIDI 1000 YAKWAMA KATIKA KIJIJI CHA SINZA BARABARA YA SOMANGA NYAMWAGE BARABARA KUU KUU YA DAR ES SALAAM, LINDI NA MTWARA.
Hapa ni Sintofahamu ya waendako ikiendelea. Msululu wa mabasi ya abiria na malori yakiwa hayajui hatma ya safari baada ya uharibifu mkubwa uliofanyika baada ya kunyesha kwa mvua kubwa za masika ambazo bado zinazoendelea kunyesha mkoani Lindi na baadhi ya maeneo nchini ,hapa ni eneo korofi la kilomita 14 kati ya kilomita 60 zinazoendelea kutengenezwa ili kukamilisha barabara hiyo ya kusini kwa kiwango cha lami.(PICHA NA MDAU PAUL MARENGA WA LINDI) Abiria mbalimbali wakiwa bado hawaelewi la kufanya kutokana na magari waliyokuwa wakiyatumia kukwama.http://dj-sek.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment