POMBE SIO MAJI !!! HUYU NI YULE MSICHANA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU DODOMA AMBAYE ALIYEJIRUSHA TOKA GOROFANI YA PILI HUKU AKIWA CHAKALI KWA MTUNGI (POMBE) NA KUUMIA KATIKA MWILI WAKE IKIWEMO PAJI LA USO.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamshna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili limetokea terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma manispaa na Mkoa wa Dodoma.Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea kuimarika
0 comments:
Post a Comment