DODOMA/DAR ES SALAAM.
WAKATI Bunge Maalumu la Katiba linatarajia kuanza kujadili Rasimu ya Katiba kesho, baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo wameanza kuondoka bungeni, kupinga mwenendo wa Bunge hilo.
WAKATI Bunge Maalumu la Katiba linatarajia kuanza kujadili Rasimu ya Katiba kesho, baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo wameanza kuondoka bungeni, kupinga mwenendo wa Bunge hilo.
Hatua hiyo ya wabunge hao inakuja wakati Bunge
Maalumu la Katiba juzi lilipitisha azimio la kutumia kura ya siri na
wazi katika kuamua vifungu vya rasimu.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba,
Samia Saluhu alisema baada ya kupitishwa kwa utaratibu wa kupiga kura za
siri na wazi katika Bunge hilo, kuanzia Jumatatu wataanza kujadili sura
ya kwanza na sita ambayo inahusu Muundo wa Muungano.
Katika sura ya kwanza, mambo ambayo yanatakiwa
kujadiliwa ni Jina, Mipaka, Alama, Lugha na Tunu za Taifa wakati sura ya
sita mambo ambayo yanapaswa kujadiliwa ni Muundo wa Muungano.
Lema atangaza kurudi jimboni Arusha
Mjumbe wa Bunge hilo, Godbless Lema alisema
anakusudia kuondoka bungeni, kutokana na kutoridhishwa na maridhiano ya
kupiga kura za siri na wazi katika kufikia uamuzi katika Bunge hilo.
Akizungumza na Mwananchi jana, Lema alisema
hakubaliani na utaratibu uliopitishwa, kwani unalenga kulazimisha kila
jambo ambalo chama tawala kinalitaka lipitishwe.
“Huu utaratibu wa kura kupigwa kwa wazi na siri
katika kitu kimoja, haupo sehemu yoyote duniani. Sasa sisi kukubali ni
kuwasaliti wananchi, kwani hata Dodoma tunaandaa rasimu ya Katiba ya
wananchi wote siyo ya CCM pekee,” alisema Lema.
Alisema pia hakubaliani na utaratibu wa kujadili
rasimu ya Katiba, ambao umetolewa na Kamati ya Uongozi kwa kuanza na
sura ya kwanza na ya sita, kwani vinalenga kufumua Rasimu ya Jaji
Warioba.
“Hapa CCM wanataka kulazimisha Serikali mbili kwa
kujadili kwanza vifungu hivi, kama vitapita basi watakuwa na uwezo wa
kubadili rasimu yote kitu ambacho mimi siwezi kukaa kwenye Bunge hili na
kusaliti wananchi waliotoa maoni kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba,” alisema Lema.
Jussa atabiri Bunge kuvunjika.
0 comments:
Post a Comment