BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ADHA YA MVUA NAMNA ILIVYOVURUGA WANANCHI WILAYA YA MVOMERO MOROGORO.


Na Mtanda Blog, Morogoro.
Wakazi wa Kata za Kanga na Pemba, wanalazimika kutumia kiasi cha kati ya Sh1,500 na  Sh2,000, kuwalipa vijana wanaofanyakazi ya kuwavusha watu katika Mto Mjonga baada ya  daraja la Maiwe ya Mamba, wilayani Mvomero kuvunjika.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, mkazi mmoja wa Turiani, Adam Muya alisema kuvunjika kwa daraja hilo kumetokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.

Muya alisema hali hiyo inawalazimisha wananchi wanaotaka kuvuka mto na kwenda upande wa pili, kulipia kiasi cha Sh1,500 na Sh2,000 kama gharama za kuvushwa.

 Kwa mujibu wa mwananchi huyo, mvua hizo pia zimesababisha huduma za usafiri wa kwenda Kibati-Turiani kuwa mgumu.

Muya alisema tatizo hilo  linatokana na daraja la Maiwe ya Mamba kumeguka na kusombwa na maji.

“Mvua za masika zimeleta kero badala ya  neema mashambani. Huku Kanga na Pemba tumekuwa tukilipa Sh1,500  na  Sh2,000 kwa sababu ya kuvunjika kwa  daraja la Mto Mjonga,: alisema Muya.

Alisema nauli ya usafiri wa pikipiki zimepanda hadi kufikia  5,000 katika baadhi ya maeneo.

Mvua hizo pia zimeleta usumbufu kwa madereva wa vyombo vya usafiri wa umma ambao wanalazimika kuegesha magari yao katika Kijiji cha Kichangani wakihofia Mto Mbulumi kujaa maji.

 Mto huo umekuwa na tabia ya kufurika maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha wakazi wa kijiji cha Kichangani na Kilimanjaro kushindwa kupita.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Wales Karia, alisema alikiri kuhusu kuwepo kwa  adha hiyo na kwamba halmashauri imeshatoa taarifa kwa Tanroads mkoani Morogoro
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: