Sehemu ya kwanza tuliishi kwa kuona namna serikali ilivyoanza kubomoa shule na wananchi kuelekeza kitongoji cha Isaka, sasa tunaenda kuona namna walivyohama na nini kiliendelea Isaka.....
Arock Athmani Usheri (74) akielezea namna walivyohamishwa
kwao alieleza kuwa walihama kwa hiyari na hali hiyo waliofia serikali kutumia
nguvu ambayo kwao ingewaletea madhara makubwa kwani wanafahamu namna serikali
inavyotumia nguvu kubwa katika mambo kama hayo.
Usheri alisema kuwa wameishi katika mapango kwa wiki mbili huku wengine
wakiishi katika mazingira hayo akiwemo, Hermani Koya, William Kilimalila na
Ibrahim Kimanga wenyewe wakiishi katika panga la Mashineni na wengine mango ya
Kipingo na Mnazi.
“Huku usafiri hakuna hata wa pikipiki wala baiskeli, mgonjwa akiumwa ni
lazima abebwe katika machela”. Alisema Usheri.
William Kilimalila na Ibrahim Kimanga wenyewe waliongeza kwa kusema kuwa
wao wanaendelea kulala katika pango hilo hadi leo na wamekuwa wakikumbana na
adha mbalimbali kipindi cha usiku.
Ibrahim Kimanga.
Anaanza kwa kusema kuwa wamekosa nafasi ya kujenga vibanda vya muda
kutokana na majukumu ya kilimo na kuhamishwa kwao kumekuwa kwa ghafla hali
iliyopelekea wao na watu wengine kukosa muda wa kujenga vibanda vya kuishi kama
wenzao na kuamua kuendelea kujisitiri katika pango hilo la mashineni kwa kulala
mpaka hapo watapoona wamepata nafasi ya kujenga vibanda vya muda.
Sehemu ya matatizo ya wakazi wa Mbangayao waliohamia kitongoji cha Isaka ambavyo hakina kabisa miundombinu ya barabara na huduma za afya.
Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha Mbangayao.
Evaresti Munyi anafafanua hali halisi ya wananchi wake kuwa baada ya
kuhama kutoka kijiji cha Mbangayao na kuhamia kitongoji cha Isaka huku akieleza
kuwa mpaka sasa kuna wananchi 19 wao bado wanaendelea kuishi katika mapango
makuu matatu huku wale waliojenga vibanda wakiishi maisha duni.
Alitaja mapango hayo kuwani ni yale ya Rock Athumani lenye watu wanne,
Mnazi watu saba na Kipingo likiwa na watu nane na kufanya idadi yao kufikia 19
wakitoka katika kaya 177 huku serikali ikitoa maturubai 20 kwa kaya 20 kwa
ajili ya kuezeka katika vibanda vya muda ili kujikinga na mvua na wakati kaya
157 zenyewe zikikosa maturubai hayo.
Munyi alisema wananchi hao wanaishi katika mazingira magumu kwa zaidi ya
mwezi mmoja tangu kuhamia Isaka na hilo linatokana na baadhi yao kushindwa
kujenga vibanda vya muda vya kuishi kama walivyofanya wenzao kutokana na sababu
mbalimbali.
“Mpaka sasa bado kuna wananchi 19 wa kijiji cha Mbangayao wanaendelea
kuishi katika mapango kitongoji cha Isaka kwa zaidi ya mwezi mmoja na siku zake
na hii inatokana na serikali kuwahamisha katika kijiji chao kwa sababu ya
kupisha hifadhi ya msitu wa Mzelezi na hali hiyo imesababisha kuibu kero
mbalimbali katika jamii hiyo”. Alisema Munyi.
Kuhamishwa huko kulikofanywa na serikali ya wilaya ya Ulanga kwanza
hakukuwa na maandalizi kwa wananchi watakofikia lakini pia hakukuzingatia hali
ya mahitaji muhimu ya kila siku ya binadamu na badala yake katika kitongoji cha
Isaka kimekuwa na ukosefu wa huduma za kijamii ikiwemo kukosa kabisa huduma ya
afya, majisafi na salama na kutokuwepo kabisa miundombinu ya barabara. Alisema
Munyi.
Kutokana na hali hiyo wananchi hao wamekuwa wakikumbwa na maradhi ya
kila aina katika maisha yao na kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata
mahitaji ya chakula katika kijiji walichohama, kutembea na wagonjwa katika
machela ya miti kwa umbali ule ule iwe asubuhi, mchana, jioni ama usiku
ilimradi tu kuifikia barabara ili kusubiri usafiri wa gari na kumpeleka
hospitali ya wilaya ya Mahenge.
Katika kile kijiji cha Mbangayao kilikuwa na kila aina ya huduma za
kijamii kwa mfano mgonjwa akiumwa alikuwa akisafirishwa muda wowote iwe kwa
pikipiki ama gari lakini maisha ya Isaka yamekuwa tofauti kwani hakuna hata
barabara na hii imekuwa kero kubwa sana kwa kila mwananchi, sasa je katika
makazi ya watu tena zenye kaya 177 hakuna barabara, maduka kwa ajili ya
mahitaji muhimu na majengo ya shule yamekuwa sio ya kuridhisha. Alisema Kaimu
Mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa maisha ya wana Mbangayao ndani ya kitongoji cha Isaka
tangu kuhamia huko hayana tofauti kabisa na maisha ya wakimbizi wengine duniani
pengine wao wanaweza kuishi maisha bora kuliko wao, kwani wakimbizi wamekuwa
wakifaidika na misaada mbalimbali lakini kwao hakuna cha msaada wa namna yoyote
kutoka kona yoyote ile ya pembe ya dunia hii inayotambua tabu ya maisha yao.
MWAJUMA KOYA KULIA NA ANNA KIALULE WAKICHOTA MAJI MTONI KITONGOJI CHA ISAKA ULANGA.
Kutokona na Hali hiyo kujitokeza kwa wananchi wa Mbangayao.
kwa kuishi kwenye mapango takribani wiki
mbili mfululizo wakiwa wamerundikana kwa kulala katika mapango hayo kwa
kuchanganyika wanawake, watoto na wanaume, ilipelekea baraza la madiwani wa
halmashauri ya wilaya ya Ulanga kuunda kamati ndogo ya madiwani wakiwemo
wataalamu toka idara ya elimu, afya na mazingira kwenda katika kitongoji hicho
cha Isaka ili kujionea hali halisi.
Kuundwa kwa kamati ndogo ya madiwani iliundwa baada ya Diwani wa kata ya
Isongo tarafa ya Vigoi, Henry Prosper Barua kuwasilisha hoja binafsi katika
kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga kwa kusema kuwa
wananchi wa Mbangayao walioamishwa na kwenda kitongoji cha Isaka kuwa wanaishi
katika mazingira magumu baada ya kuhamia kitongoji hicho na kutoandaliwa
miundombinu mbalimbali.
Barua aliyezungumza na mwandishi wa makala haya siku za mwanzo wa
kujitokeza kwa tukio hilo alimweleza mwandishi wetu kuwa katika kikao hicho cha
baraza la madiwani kilichofanyika 29 januari mwaka huu aliwatembelea
wananchi wake akiwa amebeba madawa na majisalama kufuatia kupata taarifa
za maisha wanayoishi wananchi wake na kuona wakikosa huduma muhimu za msingi
zikiwemo nyumba bora za kuishi, miundombinu ya barabara, maji, zahanati na
shule huku wakiishi katika mapango.
Baada ya Diwani huyo kuona hali hiyo alifanya vikao katika maeneo yao ya
mapango na wanafamilia zaidi ya watu 30 kwa kila pango hivyo kuliomba baraza
kuunda kamati ndogo ili kuweza kujionea hali ya maisha kufuatua kuhamishwa kwao
kwenda kitongoji cha Isaka.
Barua alifanunua kuwa zoezi la kuwaondoa wananchi hao katika kijiji cha
Mbangayao lilifanyika kwa vitisho na wananchi hao walipatwa na uoga kwa kuhofia
serikali kutumia nguvu hivyo sehemu kubwa ya watu walibomoa nyumba zao huku
nyingine zikidaiwa kubomolewa na serikali.
Kwa mujibu wa miktasali mbalimbali kijiji hicho cha Mbangayao wananchi wao
wanaishi kihalali kwani eneo hilo kutokana na kijiji kutambulika na serikali
kwa kusajiliwa toka mwaka 1954 baada ya gavana aliyetambulika kwa jina la
Robert De Stapeldon kugundua eneo hilo kuwa ni msitu wa hifadhi na kuchukua
ekari 1904 za msitu wa hifadhi na kuacha vitongoji vya Lupanga na Mbangayao.
Itaendelea kesho kuona namna maisha yanavyoendelea.
0 comments:
Post a Comment