‘Wekeza kwa maisha ya baadaye, ishinde Malaria’ hii ni kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambayo inaadhimishwa leo duniani kote.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limepanga kila ifikapo Aprili 25 kila mwaka iwe ni siku ya malaria duniani.
Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku hii kwa kuhamasisha uelewa ili kukabiliana na ugonjwa huu unaoongoza kwa kuua watu wengi.
Wataalamu wa afya wanaelezea uogonjwa wa malaria kuwa ni tishio kwa mama mjamzito na mtoto aliye bado kuzaliwa.
Takwimu za WHO zinaonyesha kwamba mwaka 2012, malaria ilisababisha vifo vya watu 672,000 duniani.
Utafiti huo unaonyesha kuwa viofo vingi ni vywa watoto na wengi ni wa Bara la Afrika.
Takwimu zinaonyesha kuwa kila baada ya sekunde 30 mtu mmoja hufariki dunia Barani Afrika.
Hapa nchini inakadiriwa kuwa kila mwaka malaria husababisha vifo vya watu zaidi ya 60,000.
Karibu aslimia 90 ya malaria inayopatikana hapa nchini ni ile isababishwayo na vimelea vya malaria aina ya plasimodium falciparum.
Aina hii ni hatari na husababisha madhara kuliko aina zingine za malaria.
Miongoni mwa madhara hayo ni kama upungufu wa damu, malaria yakupanda kichwani na madhara katika mfumo wa hewa na sukari kushuka.
Ni jambo la kawaida ugonjwa huu kuwapata wajawazito mara kwa mara kipindi cha kulea mimba kutokana na mabadiliko ya kimwili.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment