BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MADAKTARI WAFANIKIWA KUMTOA MTOTO RISASI KICHWANI KENYA.


Mtoto Satrine akiwa amepakatwa na babake.

 
Madaktari katika hospitali kubwa zaidi ya umma nchini Kenya,Kenyatta, wamefanikiwa kutoa risasi iliyokuwa imekwama katika ubongo wa mtoto Satrine Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Risasi hiyo iliyomuingia mtoto Satrine kichwani ndiyo iliyomuua mamake.

Mamake Satrine alikuwa amempakata mtoto wake ili kumlinda kutokana na magaidi waliovamia kanisa walimokuwa wiki moja iliyopita katika mtaa wa Likoni mjini Mombasa.

Lakini walimpiga risasi mama huyo na kumuua papo hapo huku risasi iliyomuua mama huyo ikiingia kichwani mwa Satrine na kukwama kwenye ubongo wake.

Satrine alipelekwa Nairobi kwa matibabu maalum kutoka Mombasa kutokana na ukosefu wa wataalamu wa upasuaji wa ubongo mjini humo.

Shughuli ya kuondoa risasi hiyo ilichukua saa tatu na ilifanywa na madaktari watatu wakiongozwa Daktari Mwangi Gichuru ambaye ni mkuu wa kitengo cha upasuaji wa neva katika hospitali hiyo.

Matoto Satrine yuko salama na daktari Mwangi anasema hawakupata matatizo walipokuwa wanafanya upasuaji huo.BBC

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: