Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyambigwa, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma mara baada ya kukagua mradi wa maji, Kinana alisema mbunge huyo amekuwa akipambana ili kukwamisha mradi huo wa maji wa Nyambigwa na kulumbana mara kwa mara na Mhandisi wa maji wa Wilaya hiyo, Mbaraka Ally kwa lengo la kutaka kumharibia kazi.
Alisema hata hivyo, mhandisi huyo alimshinda na sasa mradi huo umefikia hatua ya asilimia 90 na wakazi wa eneo hilo wameanza kupata maji.
Naye mhandisi huyo Ally, alisema mradi huo wa maji uliogharimu kiasicha Sh milioni 197, unatarajiwa kukamilika mwakani na utakuwa unazalisha lita za ujazo za maji milioni mbili wakati mahitaji ya maji kijijini hapo ni lita za ujazo za maji 203,400.HABARILEO
0 comments:
Post a Comment