BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MVUA ZILIZONYESHA KWA SIKU TATU MFULULIZO MOROGORO ZAATHIRIKA MAKAZI, MAZAO NA BARABARA.

Wakazi wa kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro wakiwa katika mafuriko kutokana na  mvua zinazonyesha na kusababaisha baadhi ya nyumba kudondoka. Picha na Mtanda Blog.

Lilian Lucas na Hamida Shariff, Morogoro.
Mvua kubwa zilizonyesha kwa muda wa siku tatu mfululizo mkoani Morogoro, zimeathiri kwa kiwango kikubwa makazi ya watu, miundombinu ya barabara na mazao ya mashambani.
Mvua hizo zilianza Alhamisi mchana na kuendelea hadi jana, zimesababisha watu 400 kukimbia makazi yao na kusimama kwa shughuli za kibiashara katika gulio maarufu la Kikundi mjini Morogoro.
Hali hiyo imetokana na maeneo ya gulio hilo kufurika kwa maji yaliyotokana mvua hizo kiasi cha kuwafanya wafanyabiashara, kufunga biashara zao.
Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wetu katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro, ulishuhudia maji ya mvua hizo yakiwa yamefurika pia kwenye nyumba za watu na kusababisha adha kubwa.
Maeneo ambayo wananchi wake wamekumbwa na mafuriko hayo ni pamoja Msamvu, Mwembesongo, Kihonda, Mafisa, Kichangani na mengine mengi.
Timu hiyo ya waandishi pia ilishuhudia baadhi ya madaraja yakiwa yamefunikwa na maji, makalavati yakiwa yamebomoka na mengine kuziba kwa magogo makubwa na takataka ngumu.
Hali hiyo imesababisha sehemu ya barabara kubomoka.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, amewahimiza wananchi kuzingatia mipango miji na kuacha kujenga mabondeni.
Alisema kufanya hivyo kitasaidia kutapunguza matukio ya mafuriko yanayosababisha hasara kubwa kwao na kwa Serikali.
Mara kwa mara, Bendera amekuwa akitoa maagizo kwa wananchi kuhama katika maeneo ya mabondeni na kuacha kuendesha shughuli za kilimo jirani na kingo za mito, ili kupuka kusababisha mito kupoteza mwelekeo wa asili na kumwaga maji katika maeneo ya makazi.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, amewahimiza wananchi kuzingatia mipango miji na kuacha kujenga mabondeni.
Alisema kufanya hivyo kitasaidia kutapunguza matukio ya mafuriko yanayosababisha hasara kubwa kwao na kwa Serikali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: