BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LIGI YA MABINGWA YA MIKOA KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO KATIKA VITUO VYA SHINYANGA, MBEYA NA MOROGORO.

 
Na Mtanda Blog, Morogoro.
Ligi ya mabingwa ya mikoa inatarajia kutimua vumbi leo katika viwanja vitatu tofauti ikijumusisha timu 27 kwa ajili ya michezo ya ufunguzi ikiwa ni kuanza kwa mbio za kusaka nafasi ya timu tatu za kucheza ligi daraja la kwanza Tanzania bara kwa msimu wa mwaka 2014/2015.


Kwa mujibu wa ratibu iliyotolewa na shirikisho la soka nchini TFF, michezo hiyo, timu zitazochuana kwa siku 36 huku kukiwa na mapumziko ya siku sita.


Vituo vya ligi hiyo ni pamoja na Morogoro, Mbeya na Shinyanga huku kila kituo kikiwa na jumla ya timu tisa.


Africab Sports ya Tanga itafungua dimba dhidi ya Kiluvya katika mchezo utaofanyika saa 8 mchana wakati saa 10 jioni Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma itayochuana na Pachoto ya Mtwara ikiwa ni michezo ya ufunguzi kwa kituo cha Morogoro kwenye jamhuri.


Katika kituo cha Mbeya, Ujenzi Rukwa itaanza kutupa karata yake na Volcano FC ya Morogoro mchezo ukitarajiwa kuchezwa majaira ya saa 8 mchana huku Arusha FC ikimenyana na Panone FC ya Kilimanjaro katika uwanja wa Sokoine.


Simiyu United FC ya Siminyu itaonyeshana kazi na Mvuvumwa FC ya Kigoma ikipigwa majira ya saa 8 mchana na Wenda FC ya Mwanza ikiteremka dimba saa 10 jioni kucheza na Eleven Stars FC ya Kagera michezo ikichezwa katika kiwanja cha Kambarage.


Kituo cha Morogoro kina timu za African Sports ya Tanga, Kilivya United FC ya Pwani, Mji Mkuu ya Dodoma, Pachoto SC ya Newala Mtwara, Bulyanhulu FC ya Shinyanga, Kariakoo FC ya Lindi, Navy FC ya Dar es Salaam, Abajalo FC ya Dar es Salaam na Mshikamano FC ya Dar es Salaam.


Kwa kituo cha Mbeya ina timu za Ujenzi FC ya Rukwa, Volcan FC ya Morogoro, Arusha FC ya Arusha, Panone FC ya Kilimanjaro, Mpanda United ya Katavi, Magereza FC ya Iringa, Tanzanite FC ya Manyara, Njombe Mji FC ya Njombe na Town Small Boys ya Ruvuma.


Kwa upande wa kituo cha Shinyanga inajumuisha timu za Simiyu United ya Simiyu, Mvuvumwa FC ya Kigoma, Wenda FC ya Mwanza, Eleven Stars FC ya Kagera, Singida United ya Singida, Mbao FC ya Mbeya, JKT Rwankoma ya Mara, Geita Veterans ya Geita na Milambo FC ya Tabora.




Mshindi wa kwanza wa kila kundi atafuzu kucheza ligi daraja la kwanza kwa msimu ujao.



Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: