BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU AAGIZA WIZARA YA FEDHA KULIPA MADENI YA WALIMU KABLA YA JUNI 30, ILI MADENI HAYO YASIINGIE KATIKA BAJETI IJAYO..

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ameiagiza Wizara ya Fedha kuhakikisha madeni ya walimu yamelipwa hadi kufikia Juni 30 mwaka huu, ili Serikali isiingie na madeni katika Bajeti ijayo.

Mbali na madeni ya walimu, Pinda alitaka pia madeni ya makandarasi, pembejeo na mengineo, kulipwa ifikapo Juni 30 kutokana na madeni kuchangia kutotekelezwa vizuri kwa Bajeti ya mwaka huu.

Pinda alisema hayo jana wakati wa kikao cha wabunge cha kupokea taarifa ya mfumo wa Bajeti kwa mwaka 2014/2015 na kutaka Wizara hiyo, kuhakikisha inalipa madeni haraka.

Alisema Bajeti iliyopita, ilikumbana na changamoto nyingi, lakini katika Bajeti ya sasa, wamejipanga kuhakikisha changamoto hizo hazijirudii na inatekelezeka, kama ilivyopangwa na kutaka wabunge kupitia maelezo ya Waziri na kuyachambua kwa makini.

“Bado Bajeti inategemea misaada kutoka nje na mikopo mpaka nchi itakapokuwa na uwezo wa kujitegemea kwani kila mwaka inapungua taratibu hasa baada ya gesi toka Mtwara kufika jijini Dar es Salaam na kuwa na umeme wa uhakika na viwanda vingi kuongeza uzalishaji,” alisema Pinda.

Pinda alisema katika kukabiliana na tatizo la mapato yasiyokuwa na kodi na katika Serikali za Mitaa kutofikiwa malengo wameunda timu maalum ya kufanyia utafiti suala hilo kwa nini hayafikii malengo na kupitia kila halmashauri kila baada ya miezi mitatu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira alisema thamani ya wazi ya utekelezaji wa miradi ya Matokeo Makubwa Sasa, imeonesha mafanikio mazuri na kukubalika kwa utaratibu huo mpya.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: