Hapa mangumi tu: Guillermo Ochoa akiokoa mpira wa hatari uliopigwa na Paulinho.
ULIKUWA usiku muhimu kwa Brazil katika mechi ya pili ya kundi A ya kombe la dunia mwaka 2014, lakini safari hii imedhihirisha kuwa si lazima wapate kila wanachokihitaji katika michuano hii.
Mashabiki wa Brazil kutoka kila kona ya nchi hiyo walifurika uwanjani kuwaona mashujaa wao na timu hiyo ya Luiz Felipe Scolari ilijitahidi kwa nguvu zote kutafuta magoli yatakayowafurahisha na hatimaye kuambulia ushindi wa pili, lakini walikumbana na kisiki cha Mpingo, Mexico.
Isingekuwa mlinda mlango wa Mexico, Guillermo Ochoa, Brazil wangebaki na furaha. Aliiokoa timu yake katika hatari mbili or tatu katika kipindi cha kwanza, lakini hatari moja ameokoa katika dakika za mwisho na kulazimisha mechi kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Ngado kwa ngado!Neymar akijaribu kuwatoka mabeki watatu wa Mexico usiku huu uliokuwa mbaya kwa Wabrazil.
Kikos cha Brazil: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Paulinho, Gustavo, Ramires (Bernard 45), Oscar (Willian 84), Neymar, Fred (Jo 68). Wachezaji wa akiba: Jefferson, Fernandinho, Hulk, Dante, Maxwell, Henrique, Hernanes, Maicon, Victor.
Kadi ya njano: Ramires
Kikosi cha Mexico: Ochoa, Aguilar, Rodriguez, Marquez, Moreno, Layun, Herrera (Fabian 76), Vazquez, Guardado, Giovani (Jiminez 84), Peralta (Hernandez 74).
Wachezaji wa akiba: Corona, Salcido, Reyes, Pulido, Ponce, Brizuela, Aquino, Pena, Talavera.
Kadi za njano: Aguilar, Vasquez.
Mwamuzi: Cuneyt Cakir (Uturuki)
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / BRAZIL WABANWA MBAVU NA MEXICO MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA KWA SARE TASA YA 0-0.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment