BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DILI LA FLORA MBASHA KUHUDUMIA KANISANI LABUMA, WACHUNGAJI WADAI HAWAWEZI KUHUDUMIWA NA MWIMBAJI MZINZI, KUTOKANA NA MPASUKO WA NDOA YAKE NA MUMEWE !!!.

Mpasuko wa ndoa ya wasanii wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha na mkewe Florah umewagawa wachungaji wa makanisa mbalimbali nchini baada ya kibao kumgeukia Flora kwamba ndiye anadaiwa kusuka mpango wa kumwangamiza mumewe ili afungwe kwa kosa la ubakaji.Wakizungumza na wanahabari wetu kwa nyakati tofauti, wachungaji hao walisema endapo itabainika ni kweli Flora ameshiriki kumsaliti mumewe kwa kutembea na mmoja wa wachungaji maarufu nchini hapatakuwa na haja ya kumwalika kwenye huduma zao kwani hawawezi kuhudumiwa na mwimbaji mzinzi.


Mchungaji Ambonile Mwakipesye na Amani Joseph wa makanisa ya Tanzania Assemblies of God ( TAG) walisema kuwa kama kulikuwa na matatizo kwenye ndoa yao walipaswa kuwaona watumishi wa Mungu na kusuluhisha badala ya kutengenezeana mitego na kuingizana majaribuni kama inavyodaiwa kutokea kwa Mbasha.


Wakati wachungaji hao wakisema hivyo, mchungaji Thomas Methew yeye alisema kuwa ukweli wa jambo hilo wanaujua wanandoa wenyewe kwani mpaka sasa hakuna anayelijua tatizo kubwa mpaka wakafikia hatua ya kutengana
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: