BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UCHOMAJI WA MIFUKO YA PLASTIKI HUSABABISHA KINGA ZA MWILI HUATHIRIN AKILI YA BINADAMU.

VIFUKO vya plastiki vilivyokamatwa vikiendelea kuteketea kwa moto, baada ya kuchomwa na kikosi kazi cha kudhibiti uingizaji na utumiaji wa mifuko hiyo, huko katika jaa la kutupia taka Vitongoji. (Picha na Abdi Suleiman,Pemba.)

Maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya vifungashio vya bidhaa viwandani, mauzo ya rejareja maduka na kwenye masoko, kumeongeza matumizi ya mifuko ya plastiki.
Ongezeko hilo hususani la mifuko maarufu kama Rambo imefanya kuongezeka kwa takataka za plastiki mijini hadi vijijini.


Hali hiyo inatokana na siku hizi bidhaa nyingi kama vile mafuta, vinywaji baridi, vipodozi, drip za hospitalini au maji ya kunywa yanayouzwa kufungwa katika mifuko ya plastiki. Bidhaa nyingi zinazotumiwa majumbani zinafungashwa katika mifuko ya plastiki au vifungashio vya plastiki ambavyo hutumiwa mara moja na kutupwa.


Hali hii imesababisha kuwepo kwa mrundikano kubwa wa taka za plastiki zinazozalishwa kwenye jamii. Wakati mwingine taka hizi huzagaa katika maeneo mbalimbali ya vijiji, miji na majiji nchini.


Kutokana na hali hiyo, mabaki ya taka za plastiki yanazusha changamoto mpya katika utunzaji wa afya ya jamii na mazingira kutokana na ukweli kuwa udhibiti wake ni mgumu na haziozi.


Watu wengi huamua kuchoma taka ngumu ikiwa ni pamoja na mabaki ya plastiki kama njia rahisi ya kufanya usafi na kudhibiti zisizagae ovyo. Wengine huchoma mifuko ya plastiki na mabaki mengine kwa ajili ya kuwashia moto wa matumizi ya nyumbani, mama na baba lishe, migahawa na sehemu mbalimbali ambazo hutumia mkaa kwa ajili ya kupika.


Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji hapa nchini, Dk Meshack Shimwela anasema kwamba, moshi unaotokana na uchomaji wa mifuko hii ya plastiki husababisha magonjwa ya mfumo wa upumuaji. Anayaelezea kwamba ni magonjwa yanayoongoza kwa kuua watu wengi katika nchi maskini duniani.


Taarifa iliyochapishwa katika gazeti hili la Mwananchi, ukurasa wa 19 toleo la Juni 6, 2014 inaonyesha uchomaji holela wa plastiki ni moja ya sababu za uzalishaji wa moshi hatari unaochafua mazingira ya hewa katika nchi zinazoendelea,Tanzania ikiwa miongoni.


Tafiti mbalimbali za kisayansi zinaonyesha kuwa, uchomaji wa plastiki kwa sababu yoyote ile, husababisha madhara kwa afya ya jamii na mazingira kutokana na kuzalisha moshi wenye sumu mbalimbali zinazochafua hewa.


Isitoshe majivu yake yana sumu hatari inayo haribu ubora wa mazingira ya maji, ardhi, mimea na chakula. Plastiki nyingi zinapochomwa huzalisha sumu kama vile dioxin, furans, caboni monoksaidi, aldehydes na polynuclear aromatic hydrocarbons (PAHs).


Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa Valavanidid A. na wenzake uliochapishwa mwaka 2008 katika jarida la malighafi hatari (Journal of Hazardous Materials) toleo la 156.


Kwa mujibu wa tafiti nyingi za afya ya jamii na mazingira, sumu hizi zimeonyesha uwezo mkubwa wa kusababisha saratani na magonjwa sugu ya mfumo wa upumuaji (OCPD) kama vile pumu, matatizo ya akili, mishipa ya fahamu pamoja na kushusha kinga ya mwili.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: