BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

EMMANUE OKWI AJISALIMISHA KWA MWENYEKITI WA KLABU YA YANGA JIJINI DAR ES SALAAM.

STRAIKA wa Yanga, Emmanuel Okwi amemtuma Mwanasheria wake afike Dar es Salaam kuteta ishu na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.


Edgar Aggaba ambaye ni raia wa Uganda, atawasili nchini kesho Jumapili tayari kutatua mzozo baina ya straika huyo na Yanga ambao msimamo wa Manji ni kutaka Okwi akatwe sehemu ya Dola 40,000 za usajili anazodai au aongeze mkataba wa mwaka mmoja.


Yanga wamefikia hatua hiyo kwa madai kuwa Okwi waliyemnunua kwa dau la Dola 100,000 lakini anawasumbua na hajafanya kazi katika miezi ya mwisho ya msimu uliopita kwa mujibu wa makubaliano.


“Nakuja Dar es Salaam wikiendi hii, naweza kuwa huko Jumapili ili mchana nikutane na Mwenyekiti wa Yanga, hii ni klabu kubwa hapa Afrika inaongozwa na viongozi makini ndiyo maana tulikubali kuwauzia Okwi, tunataka kumaliza hili tatizo kwa kutumia mazungumzo bado Okwi anataka kucheza Yanga,” alisema Aggaba.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: