BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAGE KUIACHA KLABU YA SIMBA KWA HISTORIA, WANACHAMA, WAPENZI NA MASHAKI WAKENUA MENO YA FURAHA.

 http://api.ning.com/files/KhKaa56BSVW63cGku1XoH0j4d2ulmF8aQ-Z8YO8bJfzhkj1L3-KHxXFet8UwhaZkojsWmJEtlapifOGBfmJwXmv*eW07qotb/rage22.jpg ISMAIL ADEN RAGE.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
UCHAGUZI ni habari kubwa kwasasa katika klabu ya Simba, lakini kuna maisha mengine yanaendelea ikiwemo utekelezaji wa mpango wa kujenga uwanja wa kisasa katika eneo la Bunju, jijini Dar es salaam.

Mtandao huu jana iliripoti kuwa uongozi wa Simba sc umepelekea magereda na malori ambayo kwa kutwa nzima yalikuwa yanafanya kazi ya kuondoa udongo mweusi uliopo eneo hilo na kuweka udongo mpya utakaofaa kuotesha nyasi za uwanja.

Jitihada za kuwatafuta viongozi wa Simba zilifanywa ili kupata ufafanuzi juu ya suala hilo na mtandao huu umejitahidi kumtafuta rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage ili kutoa ufafanuzi wa zoezi hilo na pesa zimepatikana wapi wakati huu Simba ikitarajia kufanya uchaguzi juni 29 mwaka huu.


Kuna watu walihusianisha mpango huo na kampeni kuelekea uchaguzi. Kuna wagombea fulani (majina tunayo) walikuwa wanahusishwa na kutoa fedha hizo ili kujisafishia njia, lakini halikuwa jibu sahihi na ikabidi Rage asakwe ili atoe maelezo.


Katika mahojiano yake na mtandao huu, Rage amesema sasa wameshaanza mambo baada ya kupata fedha mahali fulani (hakutaka kutaja) na suala la wanachama kwenda na majembe, mapanga wameacha.


“Uko katika hatua nzuri kuna kitu ambacho wataalamu wa udongo wanaita, wametoa ule udongo mweusi, wameanza kuweka udongo ambao utafaa kupandia nyasi za uwanja”. Alisema Rage. 


‘Na kama unakumbuka mara ya kwanza tulipoanza kukarabati au kuujenga, tuliwaomba wanachama, wakaenda na mapanga na majembe.”


“Sasa tumeacha, kwasababu tulipata pesa mahali fulani, sasa kuna magereda na malori yanafanya kazi ya kutoa huo mchanga ambao haufai na kuweka mchanga unaofaa kwa kuotesha nyasi”. Aliongeza Rage.


Rais huyo aliyekuwa na mvutano mkali na wanachama wa Simba pamoja na viongozi wenzake wakati wa uongozi wake alisema ndani ya siku chache zijazo watawakaribisha waandishi wa habari ili wakapige picha, waone uwanja ulivyokuwa mzuri, ulivyopendaze na hatua nzuri ambazo wanazo.


Hata hivyo, Rage alisema wamechoshwa na kutumia gharama kubwa za kuweka kambi Hotelini, hivyo anataka kujenga Hosteli za wachezaji kabla hajakabidhi madaraka kwa uongozi mpya.


“Lakini ninafanya vilevile mpango, kwasababu tunatumia gharama nyingi sana kuwaweka wachezaji wetu Hotelini wakati tunapofanya kambi”.


“kwasababu eneo hilo ni zuri, tunataka ikiwezekana kabla sijaondoka, angalau nipate michoro au niweze kuweka msingi au ghorofa moja ikibidi, tujenge hosteli katika muda huu mfupi uliobaki”. Alisema Rage.


Kuhusu usajili, Rage alisema anataka kuweka rekodi ambayo haijawahi kutokea Simba ambapo atawaachia viongozi wajao kitita kirefu cha pesa, si chini ya milioni 300 kwa ajili ya usajili.


“Sasa hiyo nawaachia viongozi wajao ambao ninakusudia kuweka rekodi ambayo haijatokea Simba tangu miaka yote, kwa maana ya kwamba nitakapoondoka mimi nitawaachia pesa za wao kufanya usajili si chini ya milioni 300 watazikuta pale klabu”.


“Sivyo kama mimi nilipoingia sikukuta hata shilingi moja nilikuta madeni basi, hiyo ndiyo nataka niweke tofauti yangu mimi ambaye ninaithamini klabu yangu hii”. Alieleza Rage.


Nako upande wa pili, mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameongezewa muda wa mwaka mmoja na wanachama wa Yanga ili kukamilisha baadhi ya ahadi zake ikiwemo ujenzi wa uwanja wa kisasa maeneo ya Jangwani.


Hatua za Simba zinaweza kumshitua na akaongeza kasi.
Simba na Yanga ni klabu kongwe ambazo hazina hata uwanja wa mazoezi.


Azam fc ni klabu pekee yenye uwanja wake wenye ubora wa kimataifa uliopo Mbande, chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.


Mbeya City fc ambao wameshiriki kwa mara ya kwanza ligi kuu msimu uliopita, wana mpango wa kujenga uwanja wao maeneo ya Iwambi jijini Mbeya. - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2075#sthash.QnOc6Vtc.dpuf
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: