BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HII HAIINGII AKILINI HATA PUNJE, ETI BIBI WA MTOTO NASRA ALIYEISHI KATIKA BOKSI KWA MIAKA MINNE AIBUKA NA KUTAKA MWILI WAKAZIKE, USTAWI WA JAMII WAMTOLEA NJE MOROGORO.a boksi' aibuka


WAKATI mtoto Nasra Mvungi (4), aliyeteswa na walezi kwa kuishi katika maboksi kwa zaidi ya miaka mitatu, akitarajiwa kuzikwa leo, bibi mzaa mama yake, Asha Abdalah, aliibuka jana kuomba mwili wa marehemu ili wakazike nyumbani kwao.

Huku akiwa amefuatana na wajomba wa Nasra, bibi huyo alifika katika ofisi za Ustawi wa Jamii na kuomba mwili wa marehemu ili wakazike nyumbani kwao.

Walipoulizwa walikuwa wapi siku zote wakati mtoto huyo akiteseka na hata alipokuwa hospitali, waliamua kutoka nje ya ofisi hiyo na baadaye kurudi na hoja ya kutaka kuonana na Ofisa Ustawi wa Jamii kwa mazungumzo.

Taarifa kutoka katika ofisi hiyo, zilieleza kuwa bibi huyo na wajomba, walijibiwa kuwa ofisa wanayemhitaji yupo katika Kituo cha Polisi na kama wanahitaji wafike katika kituo hicho, walipata wasiwasi na kuamua kuahirisha matakwa hayo.

Baada ya kuahirisha kuomba mwili na kumuona ofisa huyo, bibi huyo aliomba ofisi hiyo impe fursa ya kuwa katika watakaohudhuria maziko hayo leo.

Wakati huo huo, mwili wa Nasra ambaye alifariki dunia juzi saa saba na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya hali yake kubadilika ghafla na madaktari kumuwekea mashine za kumsaidia kupumua, uliwasili jana mkoani hapa kutoka Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Afya wa Ustawi wa Jamii mkoani hapa, Yoranda Mkapa, ambaye pia ni mratibu wa maziko hayo, aliwashukuru wadau kutoka katika taasisi mbalimbali waliojitokeza kusaidia kusafirisha mwili wa Nasra kutoka jijini Dar es Salaam hadi Morogoro.

Mwili wa mtoto huyo ulipelekwa moja kwa moja katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa na leo saa moja asubuhi, utapelekwa katika Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa sala na baadaye katika Uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kuuaga kabla ya kwenda katika makaburi ya Kola kwa ajili ya maziko.

Wakizungumzia kifo hicho, baadhi ya wananchi mkoani hapa walielezea kusikitishwa na taarifa, huku wengine wakisema walitamani mtoto huyo akue ili waliomfanyia ubaya waone aibu.

Walisema kuwa kitendo cha kumhifadhi mtoto ndani ya boksi kama msukule pasipo kupewa huduma zozote za kiafya si kizuri na kimewadhalilisha.

Akizungumza mara baada ya kuhifadhi mwili wa Nasra hospitalini, Ofisa Ustawi wa Jamii mkoani hapa, Oswin Ngungamtitu, aliwashukuru majirani, Mwenyekiti wa Mtaa pamoja na Ofisa Mtendaji kwa kufichua mateso ya mtoto huyo.

Pia aliwashukuru waandishi wa habari kwa kuandika habari za mtoto huyo na kusaidia jamii na Taifa kwa ujumla kujua ukatili aliofanyiwa mtoto huyo. Hata hivyo Ngungamtitu aliiasa jamii kuacha kutoka nje ya ndoa na kujiepusha na tabia ya kuwanyanyapaa watoto kwa kigezo cha ulemavu.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: