BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIVI NDIVYO MKUU WA MKOA MOROGORO NA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI WALIVYOONGOZA MAMIA KATIKA MAZISHI YA MTOTO NASRA RASHID ALIYEISHI KATIKA BOKSI KWA MIAKA MINNE KUANZIA MSIKITI MKUU, JAMHURI HADI MAKABURI YA KOLLA.


Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifafanua jambo juu ya maisha ya mateso ya mtoto Nasra wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu mtoto huyo katika uwanja wa jamhuri kisha mwili wake kupelekwa katika msikiti kuu wa mkoa wa Morogoro kwa kumswalia kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Kolla mkoani hapa. PICHA/MTANDA BLOG.

Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akizungumza jambo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu mtoto Nasra katika uwanja wa jamhuri kisha mwili wake kupelekwa katika msikiti kuu wa mkoa wa Morogoro kwa ajili ya sala ya kuambezi kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Kolla mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
Kaimu Sheikhe wa Bakwata mkoa wa Morogoro Ally Mohamed akitoa ufafanuzi wa jambo.PICHA/MTANDA BLOG.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera wa pili kutoka kushoto, Kaimu Sheikhe wa Bakwata mkoa wa Morogoro Ally Mohamed wa kwanza kushoto wakiwa katika shughuli hiyo.PICHA/MTANDA BLOG.
Jeneza lenye mwili wa mtoto Nasra likiwa wasili katika uwanja wa jamhuri ikitokea msikiti kuu wa mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuagwa.PICHA/MTANDA BLOG.
Joel Bebdera akiteta jambo na Afisa wa Ustawi wa jamii mkoa wa Morogoro Oswin Ngungamtitu kulia.
PICHA/MTANDA BLOG.


Kaka wa Nasra akiwa amejiinamia kwa kuwaza jambo wakati wa matukio mbalimbalin yakiendelea.PICHA/MTANDA BLOG.
 
Kaimu Sheikhe wa Bakwata mkoa wa Morogoro Ally Mohamed wa kwanza kushoto mstari wa mbele akiwaongoza waumini wa dini ya kiisla kuomba dua bara baada ya kumaliza swala ya kumswalia Nasra katika msikiti mkuu wa mkoa wa Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
 
Waumini wa dini ya kiislam wakiwa wamebeba sanduku kenye mwili wa marehemu Nasra kuelekea makaburini Kolla kwa ajili ya maziko. PICHA/MTANDA BLOG.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini kupitia kitiki ya CCM Abdullaziz Mohamed Abood kushoto akiwaongoza wananchi waliojitokeza katika mazishi ya Nasra kubeba jeneza katika makaburi ya Kolla.PICHA/MTANDA BLOG.
 Shughuli ya mazishi zilikuwa hivi.PICHA/MTANDA BLOG.
Bendera akichota mchanga na kuingiza kaburini.PICHA/MTANDA BLOG.
Abood anaye alifuatia kwa kitendo hicho.PICHA/MTANDA BLOG.
Sehemu ya umati wa wananchi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake katika makaburi ya Kolla wakati wa mazishi hayo.PICHA/MTANDA BLOG.
Abood akiteta jambo na Kaimu Sheikhe wa Bakwata mkoa wa Morogoro Ally Mohamed na kutangaza kusoma hitima ya mtoto huyo itayofanyika siku ya juni 14 mwaka huu uwanja wa jamhuri Morogoro. PICHA/MTANDA BLOG.
Hapa dua ikiombwa baada ya shughuli ya mazishi kumalizika.PICHA/MTANDA BLOG.
 
Bendera akisistiza jambo na kutoa shukurani kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza katika mazishi hayo.PICHA/MTANDA BLOG.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: