BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ITALY NA IVORY COAST OUT KATIKA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014.

Italy's Andrea Barzagli tackles Uruguay's Luis Suarez
Kwa mara nyingine katika kipindi cha maisha yake ya soka, Luis Suarez ameingia tena kwenye headlines kwa kumng’ata mchezaji mwenzie uwanjani.
Kwenye mchezo wa mwisho wa makundi kati ya Uruguay vs Italy, zikiwa zimebakia dakika 9 mchezo kuisha ulitokea utata mkubwa wakati Suarez na Chiellini walipokumbana katika maeneo ya penalti
20140625-081301-29581417.jpg
Beki huyo wa Italia alilalamika wakati kwa refa kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.

Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.

Mpaka unamalizika Uruguay walikuwa washindi, na kuungana na Costa Rica kwenda hatua ya 16 ya michuano hiyo.



Wakati huo huo Italy iliungana na England iliyomaliza mechi zake za makundi kwa kutoka sare ya 0-0 na costa Rica – kufungasha virago kurudi nyumbani zikishindwa kufuzu kwenda hatua ya pili.
Uruguay sasa itacheza na Colombia wakati Costa Rica ikikutana na Ugiriki kwenye hatua ya 16 bora.


IVORY COAST 1-2 UGIRIKI.


Matumaini ya bara la Afrika kuingiza timu kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia yameanza kupotea.

Wakicheza mchezo wao muhimu na wa mwisho, Ivory Coast ilikubali kipigo kutoka kwa Ugiriki katika mchezo ulioisha kwa kufungwa 2-1.

Kufuatia ushindi huo Ugiriki imeungana na Colombia kwenda hatua ya pili kutoka kwenye kundi hilo.

Ugiriki ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia bao la kwanza la Georgios Samaras kunako dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinzi wa Ivory Coast Cheick Tiote kufanya makosa ya kipuuzi.

Ivory Coast hata hivyo ilifunga bao la kusawazisha kupitia Wilfried Bony aliyetumia vyema pasi safi kutoka kwa Gervinho.

Ugiriki walipata goli la kupitia penati ya dakika za majeruhi iliyofungwa na Samaras tena.

JAPAN 1-4 COLOMBIA.

Colombia ilikamilisha mechi za makundi kwa kuiadhibu Japan 4-1 na kuweka rekodi ya kushinda mechi zote katika makundi.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: