MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Ernest Mangu, amepiga marufuku
vikundi vya ngoma vya Kigodoro, Kangamoko na vingine vinavyokiuka
maadili ya kitanzania.
Kutokana na hatua hiyo, IGP Mangu amewaagiza Makamanda wa Polisi wa
mikoa yote nchini kuhakikisha wanadhibiti vikundi hivyo vinavyodaiwa
kuwa chanzo cha matukio mbali mbali ya kihalifu na kuporomosha maadili.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji
wa Jeshi la Polisi nchini SSP Advera Senso, kwa niaba ya IGP Mangu,
alisema vikundi hivyo vinatakiwa kufuata taratibu zinazowekwa na
halmashauri zao pasipo kukiuka maadili.
Alisema licha ya vikundi hivyo kufanya vitendo vya kukiuka maadili ya
kitanzania pia wakati wa ngoma hizo wahusika wamekuwa wakifunga
barabara na kufanya uhalifu katika maeneo wanayofanyia burudani zao hali
inayosababisha usumbufu mkubwa kwa watu wengine.
“Hatupingi ngoma za asili bali tunakataa vitendo vinavyodhalilisha
utu wa binadamu hasa mwanamke na maadili ya kitanzania, vinalindwa. Hili
sisi kama jeshi hatuwezi kulivumilia,”alisema Senso.
Alisema hata matukio mengi ya kihalifu yanayohusisha makundi ya
kihalifu kama Panya Road, Mbwa mwitu na Machizi sabini ni matokeo ya
ngoma hizo zinazokesha kwa kucheza nusu uchi.
Juni 18 mwaka huu wacheza ngoma wawili wa kundi la Kangamoko wakazi
wa Mwananyamala, walijeruhiwa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni
askari baada ya kutokea vurugu za kuwazuia askari wasitekeleze wajibu
wao wa kuzuia ngoma hizo kama zilivyotangazwa na mamlaka husika.
Mbali na kupiga marufuku ngoma za vigodoro, Senso alisema Polisi
imeanzisha operesheni maalum ya kuwadhibiti madereva piki piki, bajaji,
guta na baiskeli wanaokiuka sheria za barabarani na kusababisha ajali za
mara kwa mara na kuathiri nguvu kazi ya taifa.
Alisema miongoni mwa makosa yanayofanywa na madereva wa vyombo hivyo
ni pamoja na kutozingatia alama na michoro ya usalama barabarani, kupita
taa nyekundu inayoawaashiria kusimama pamoja na kuendesha piki piki zao
kwa mwendo wa hatari, jambo aliloeleza kuwa ni kinyume na sheria za
usalama barabarani.
Katika siku za hivi karibuni baadhi ya vikundi vya ngoma
vinavyojitambulisha kwa majina kama Vigodoro, Kanga moko (Ndembendembe
laki si pesa), Kantangaze na Bunyero bunyero inayochezwa kwenye baadhi
ya kumbi maarufu za burudani, vimekuwa vinara wa kukiuka maadili ya
kitanzania kwa kucheza wakiwa uchi.
Kutokana na uchezaji huo wa kukiuka maadili mijadala mbali mbali ya
namna vikundi hivyo vinavyochangia kuporomosha hadhi ya mtanzania hasa
wanawake, zimekuwa zikijadiliwa hata kufikia hatua ya bunge kuhoji hali
hiyo.
Wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kwa mwaka wa fedha 2014/15, baadhi wabunge waliihoji serikali
kwanini imekaa kimya wakati utamaduni wa kitanzania umekuwa ukipotoshwa
hadharani pamoja na kuchochewa kwa hisia za ngono na makundi hayo.TANZANIA DAIMA
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / JESHI LA POLISI LAPIA MAFURUKU VIKUNDI VYA KANGAMOKO NA KIGODORO, KISA NI.......
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment