BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KESI YA MTOTO NASRA, MTUHUMIWA AANZA VITUKO MAHAKAMANI MOROGORO.

Omari Mtonga (30) aliyejifunika fulana usoni na Rashid Mvungi wakiwa chini ya ulinzi wakati wakielekea katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi Morogoro kusikiliza mashtaka yanayowakabili yanayowakali juu ya kesi ya mtoto Nasra Mvungi mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG

Mtuhumiwa wa kesi ya mtoto Nasra Mvungi, Mariam Said akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi wakati akisindikizwa kwenda mahakama ya hakimu mkazi Morogoro kusikiliza mashtaka yanayomkali mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
Kutoka kushoto Mariam Said, Rashid Mvungi na Omari Mtonga wakiwa katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro muda kabla ya kusikiliza kesi yao inayowakali ya mtoto Nasra Mvungi mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG


Kesi ya watuhumiwa watatu wa unyanyasaji na kusababisha kifo cha mtoto Nasra Rashidi (4) imeahirishwa hadi Julai 10 mwaka huu, kufuatia upelelezi wa shauri hilo kutokamalika.
Wakili wa Serikali, Sunday Hyera, kwa kushirikiana na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Zabron Msusi, jana waliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro kupanga tarehe ya kutajwa tena shauri hilo kufuatia upelelezi wake kutokamilika.

Hakimu Mary Moyo, alikubalina na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 10 mwaka huu.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana majira ya saa 3 asubuhi wakitokea mahabusu wakiongozwa na  baba mzazi wa mtoto huyo Rashid Mvungi (47) mkazi wa Lukobe pamoja na wanandoa Mariam Said (38) na Mtonga Omari (30), wote wakazi wa mtaa wa Azimio, kata ya Kiwanja cha Ndege, mkoani hapa.

Watuhumiwa wote walirudishwa rumande kutokana na kukabiliwa na shitaka la mauaji ambalo halina dhamana na mahakahama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Katika keshi hiyo, awali watuhumiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama na kutenda ukatili dhidi ya mtoto Nasra.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mei 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro baada ya mtoto huyo kufariki na watuhumiwa hao kubadilishiwa mashtaka na kusomewa la kusababisha mauaji. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: