Mwanasheria wa mwanamke wa Sudan aliyekamatwa siku
chache baada ya kuachiwa baada ya kuhukumiwa kifo kwa kuasi dini ya
Kiislam kwa kuolewa na Mkristo, amesema mteja wake anatuhumiwa kwa
kughushi nyaraka za safari.
Amesema mwanamke huyo Meriam Ibrahim bado anashikiliwa katika kituo cha polisi katika mji Mkuu wa Khartoum.
Sudan Kusini ambayo ndio iliyompa nyaraka hizo imesema kuwa nyaraka hizo ni halali kwa vile ameolewa na mwanaume raia halisi wa Sudan Kusini.
Mwanasheria wa Meriam Ibrahim amesema yeye pamoja na mumewe walikuwa wakiohojiwa kuhusuana na hati za kusafiria. Ilikuwa inasadikiwa kuwa walikuwa wanasafiri kuelekea nchini Marekani.
Mwanamke huyo Meriam Ibrahim, alihukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu alikamatwa akiwa na familia yake katika uwanja wa ndege mjini Khartoum.
Watu waliomkata walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia ingawa wanaaminika kuwa wanajeshi wa serikali.
Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.
Haijulikani kwa nini alikamatwa na karibu watu arobaini waliokuwa wamavalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya kuachiliwa kuambatana na uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Alikamatwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela punde baada ya kuhukumiwa.
Familia yake imepelekwa katika makao makuu ya idara ya ujasusi.
Kabla ya kuzuiliwa kwaketena, jamii ya kimataifa yalipongeza uamuzi wa kuachiliwa kwake na kumuondolea hukumu ya kifo chake.BBC
0 comments:
Post a Comment