BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTOTO NASRA ALIYEFARIKI DUNIA JUNI MOSI AZIKWA KISHUJAA, NI YULE ALIYEISHI KATIKA BOKSI KWA MIAKA MINNE MANISPAA YA MOROGORO.


Wananchi wa mji wa Morogoro wakifuatilia mwenendo wa shughli ya kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Nasra Rashid (4) katika uwanja wa jamhuri Morogoro, kabla ya mazishi yaliyofanyika jana. Picha na Juma Mtanda.

Mtoto huyo aliyefariki akiwa na umri wa miaka minne, alifariki Juni Mosi kwenye Hospitali ya Muhimbili kutokana na maradhi ya homa ya mapafu. Aliishi kwenye boksi tangu alipokuwa na umri wa miezi tisa.

Watu katika mazishi hayo walianza kujitokeza kwenye Uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 1:00 asubuhi na mwili huo ulifikishwa uwanjani hapo saa moja baadaye.


Baada ya mwili wa marehemu kuingizwa katika uwanja huo vilio vilisikika kutoka kwa watu mbalimbali zaidi kina mama na wanafunzi wa shule za msingi wakiimba... “Tuna imani na Mahakama, tuna imani na sheria.”


Wakati salamu mbalimbali zikitolewa, baba mzazi wa Nasra, Rashid Mvungi alikuwa ameinamisha kichwa huku akitokwa na machozi.


Kabla ya shughuli ya kutoa heshima za mwisho kuanza, bibi wa marehemu, Asha Abdallah aliingia uwanjani hapo akilia na kuomba kukaa meza kuu ili ashuhudie shughuli za kumuaga mjukuu wake.


Baada ya mwili wa mjukuu wake kuondolewa kupelekwa makaburi ya Kola, bibi huyo alianza kueleza namna alivyoupokea msiba huo akisema kwa kipindi chote Nasra alipochukuliwa na mama yake mkubwa, hakuwahi kumuona mjukuu wake.


“Mariamu (mama mkubwa wa Nasra) ni mtoto wangu lakini baada ya kumchukua Nasra nilikuwa nikimwambia kila siku niletee mjukuu wangu nimuone au njoo unichukue nikamwone mjukuu wangu lakini alikuwa akiniahidi kesho mara kesho kutwa na mimi nilikuwa sipajui nyumbani kwake,” alisema bibi huyo.


Hata hivyo, alielezea kusikitishwa na hatua ya Serikali kuamua kumzika mjukuu wake bila ya kumshirikisha akisema hana hatia kwani alitamani kumlea lakini Mariamu alimchukua naye aliamini kuwa angemlea vizuri.


Mazishi hayo yalihudhuriwa pia na kaka wa marehemu, Nasoro Mahamba aliyekuwa amesindikizwa na shangazi yake, Tatu Mahamba. Nasoro alisema tangu akiwa na miaka minne alikuwa akiishi na shangazi yake huyo na alikuwa akienda kumtembelea marehemu mama yake wakati wa likizo tu.


Nasoro alisema alipoteza mawasiliano na mama yake mkubwa na kushindwa kujua jinsi ya kumwona mdogo wake.


Nasoro alisema siku ambayo Nasra alipelekwa Muhimbili alikwenda Hospitali ya Morogoro lakini alishindwa kuzungumza naye kutokana na hali yake kuwa mbaya.


Hata hivyo, Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Kihonda, alishindwa kufika makaburini kumzika mdogo wake akisema anasumbuliwa na tatizo la moyo hivyo kuhofia kuanguka.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: