BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MUME WA FROLA MBASHA APATA DHAMANA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM


NA KULWA MZEE
MUIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha (32), jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji.

Mbasha, ambaye pia ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha, alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Wilberforce Luago.

Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai mshtakiwa ambaye pia ni mfanyabiashara, alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.

“Mheshimiwa hakimu, mshtakiwa katika shtaka la kwanza anadaiwa Mei 23 mwaka huu, maeneo ya Tabata Kimanga wilayani Ilala, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa, alimbaka shemeji yake (jina tunalo).

“Katika shtaka la pili, mshtakiwa unadaiwa kwamba, Mei 25 mwaka huu maeneo ya Tabata Kimanga kinyume cha sheria, ulimbaka tena mfanyakazi wako,” alidai Katuga.

Mshtakiwa alipotakiwa kujibu kama kweli au si kweli, alikana kutenda makosa hayo, mahakama ilikubali kumpa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe ametoka katika taasisi ya serikali inayotambulika.

“Mshtakiwa ili adhaminiwe anatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe ametoka katika taasisi ya Serikali inayotambulika, wasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tano,” alisema.

Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, kesi iliahirishwa hadi Juni 19 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama ametimiza masharti ya dhamana.

Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa Polisi alisindikizwa katika basi la Magereza kwa ajili ya kwenda mahabusu Keko, jijini Dar es Salaam.

Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa Polisi alisindikizwa katika basi la Magereza kwa ajili ya kwenda mahabusu Keko, jijini Dar es Salaam.

Mbasha alivalia suruali ya rangi ya Ugoro na shati la rangi ya damu ya mzee huku akiwa na Kandambili miguuni, tofauti na alivyozoeleka machoni mwa watu, ambapo mara nyingi amekuwa akivaa nadhifu.

SAKATA LA MBASHA KUBAKA
Taarifa za Mbasha kubaka liliibuka rasmi mwishoni mwa mwezi uliopita, ambako baadhi ya vyombo vya habari nchini pamoja na mitandao ya kijamii vililiripoti tukio hilo.

Mei 30 mwaka huu, Jeshi la Polisi, kupitia kwa Kamanda wake wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi, lilithibitisha kupokea tuhuma dhidi ya Mbasha na kueleza kuwa Jeshi lake linamsaka.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliokuwa karibu na Mbasha walidai kuwa tukio hilo lina msukumo wa ugomvi wa kifamilia kati ya Mbasha na mkewe na kwamba chanzo cha ugomvi huo ni mali.

Ilifikia hatua ya kuwapo kwa madai ya wawili hao kuishi mafichoni kutokana na tukio hilo, pia kuliibuka taarifa za Flora kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na ilidaiwa kuwa Jeshi la Polisi lilimuokoa.

Akizungumzia tukio hilo la kuvamiwa Frola alinukuliwa akisema tukio hilo limemfanya kuwa na hofu na kwamba watu hao walikuwa wakimfuatilia kwa karibu kila sehemu.

“Unajua kwa sasa nina hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa karibu kila sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi na sijui lengo lao.”alisema.

Binti anayetajwa kubakwa na Mbasha anadaiwa kuwa ni yatima.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: