Daktari wa watoto mapacha waliokuwa wameungana akiwa amewabeba mara baada ya kufanywa upasuaji hivi karibuni.
Dar es Salaam.
Hatimaye mtoto Eliud, mmoja kati ya pacha waliokuwa wameungana kabla ya kutenganishwa kwa upasuaji huko India Februari, mwaka huu, ameanza kwenda haja kubwa kwa njia ya kawaida baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo na kurudishwa ndani sehemu ya utumbo iliyokuwa imetoka nje.

Upasuaji huo ulifanywa Ijumaa iliyopita katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na jopo la madaktari bingwa kutoka
Misri.Baada ya kurejea kutoka India na kisha kwenda Mbeya, Eliud alipata
tatizo la utumbo mkubwa kutoka nje na kutopenda kula, hali iliyomfanya
adhoofu.
Jana, baba mzazi wa pacha hao, Eric Mwakyusa
alisema upasuaji huo ulifanikiwa na sasa mtoto huyo anaendelea vizuri...
“Ninamshukuru Mungu sasa Eliudi anakula na kwenda haja kubwa kwa njia
ya kawaida. Kwa sasa tunauguza kidonda tu.”
Daktari anayewasimamia watoto hao, Zaituni Bokhary
hakupatikana kuzungumzia hali za pacha hao lakini Mwakyusa alisema
madaktari hao wako karibu na pacha hao kujua maendeleo yao.
Mwakyusa alisema pacha mwingine, Elikana ambaye
pia alikuwa na tatizo la utumbo kutoka nje kwa kiasi kidogo
ikilinganishwa na Eliud, atafanyiwa upasuaji... “Kurudisha utumbo ndani
na kuziba tundu.”
Watoto hao wanatarajiwa kurejea India Agosti, mwaka huu kwa ajili ya upasuaji mwingine.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment