BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PROFESA LIPOUMBA NA MAALIF SEIF WAENDELEA TENA KUIONGOZA CUF.

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amechaguliwa tena kuendelea na wadhifa huo.
Ingawa matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa leo, lakini taarifa za awali tulizozipata wakati kazi ya kuhesabu kura ikiendelea, zinaonyesha kuwa Profesa Lipumba anaongoza.

Katika uchaguzi huo, Profesa Lipumba alipata upinzani kutoka kwa makada wengine wawili ambao ni Chifu Yemba wa mkoani Shinyanga na Adam M’bezi wa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa matokeo hayo yasiyo rasmi, Juma Duni Haji amerejea kwenye nafasi yake ya makamu mwenyekiti wa chama hicho taifa baada ya kumshinda mpinzani wake, Haji Kombo.

Mbali ya Lipumba na Duni kurejea kwenye nafasi zao, Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad naye pia ametetea kiti chake baada ya kupita bila kupingwa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari, Abdul Kambaya, matokeo kamili ya uchaguzi yatatangazwa leo mbele ya wanahabari.

CUF pia imefanya uchaguzi wa wanawake kutoka Zanzibar ili kupata asilimia 30 ya wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa.

Uchaguzi huo utaendelea leo kwa kuchaguliwa wajumbe wa Baraza Kuu kanda saba za Bara.

Wakati huo huo, Baraza Kuu la CUF, limefanya mabadiliko ya katiba yake kwa kuingiza kipengele cha Kamati ya Maadili ambacho hakikuwemo kwanye katiba ya awali.

Kambaya aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa lengo la kamati hiyo ni kusimamia maadili na utendaji kazi wa viongozi wa chama hicho.

Kamati hiyo itaongozwa na wajumbe saba kutoka pande zote mbili, yaani Tanzania Bara na Visiwani ambao ni Makamu Mwenyekiti, Katibu wa Ulinzi na Usalama na naibu wake.

Wengine ni wajumbe wanne ambao ni wanawake wawili kutoka Bara na wengine wawili kutoka Zanzibar.

Alisema mkutano huo umepinga mapendekezo ya kuwa na uongozi wa mkoa kwa sababu kwa kufanya hivyo kungekiongezea chama gharama wakati bado kichanga kifedha.

Kambaya aliongeza kuwa mkutano huo umekubaliana kuanzisha tena uongozi wa jimbo ili kukiwezesha chama kushiriki vizuri uchaguzi wa uwakilishi wa majimbo.

Pia alisema mkutano huo umepinga uteuzi wa makatibu wa wilaya kufanywa na Baraza Kuu ili uteuzi wake ufanyike katika ngazi ya wilaya.TANZANIA DAIMA
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: