Na Mtanda Blog, Dodoma.
Timu nne za soka za kanda ya mashariki zimefanikiwa kuvuka na kutinga hatua ya ligi ndogo ya mashindano mapya ya castle lager perfect 6 2014 kwa mikoa ya Morogoro na Dodoma.
Katika michezo ya hatua ya mchujo ikirishikisha timu nane za mikoa hiyo, kwa upande wa Morogoro timu za Mzinga FC na Ndezi FC zenyewe zilikata mapema tiketi ya kucheza ligi hiyo huku kwa Dodoma ikiwa ni Schalk 04 FC pamoja na Market FC.
Schalk 04 na Market FC zilikata tiketi juzi kwa kushika nafasi ya kwanza na pili katika uwanja wa Central msikiti wa Gadaff mjini Dodoma baada ya kuvuka katika hatua ya mchujo wakati Ndezi FC na Mzinga FC zikifanya hivyo katika michezo iliyofanyika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Mtaribu wa mashindano hayo castle lager perfect 6 2014 kanda ya mashariki, Ibrahim Kyaruzi alisema kuwa baada ya kumalizika kwa hatua ya mchujo kwa michezo iliyofanyika Morogoro na Dodoma inayounda kanda ya mashariki na kupata timu nne, timu hizo zitacheza ligi ndogo ili kupata timu moja itayowakilisha kanda ya mashariki katika mashindano hayo ya taifa jijini Dar es Salaam.
Kyaruzi alisema kuwa ligi ndogo itafanyika juni 7 mwaka huu Manispaa ya Morogoro kwa kuzikutanisha washindi wa kwanza wa Dodoma ambazo ni timu za Schalk 04 na Market FC na Ndezi FC na Mzinga FC ili kucheza na kupata mshindi wa kanda ya mashariki atayewakilisha kanda hiyo kwenye mashandano hayo jijini Dar es Salaam.
“Haya mashindano ni mapya lakini lengo lake ni kutoa fursa kwa vijana waliokosa nafasi ya kucheza soka katika ligi mbalimbali za hapa Tanzania kuibukia katika mashindano haya na licha ya faida hiyo mshindi wa kwanza atapata nafasi ya kudhaminiwa bia catle lager ya kupitia castle lager ambayo itaghalamia safari ya kwendaa na kurudi nchini Hispania kwa wachezaji sita kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona.”alisema Kyaruzi.
0 comments:
Post a Comment