Ulaji wa kuku wa kisasa au broila’ umeelezwa na wataalamu kuwa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la maradhi ya saratani nchini.
Kitoweo hicho kinasababisha kansa kwa vile ndege hao hulishwa vyakula
kama karanga, mahindi, mashudu na dagaa ambazo vina sumu ya
‘mycotoxin’ inayotokana na fangasi ambayo inachochea ukuaji wa seli za
saratani mwilini.
Mshauri wa Mifugo wa kampuni ya Bytrade Tanzania , Omari Magoma, alitoa
tahadhari hiyo katika mahojiano maalum ya NIPASHE Jumamosi, kuhusu
ugonjwa huo na kufahamisha kuwa tatizo la kansa ya kuku linaendelea
kuongezeka kila siku lakini likiwashambulia walaji na kukuza ukubwa wa
kansa nchini.
Alisema ugonjwa huo ambao upo kwa muda mrefu kwenye miili ya kuku
unasambaa sehemu zote mwilini mwake na pindi mlaji anapokula kitoweo
hicho mara nyingi anaambukizwa maradhi ya kansa.
“Sumu ya mycotoxin huzalishwa na fangasi kutoka kwenye chakula kama
mahindi, mashudu, karanga na dagaa vyakula ambavyo wafugaji huwalisha
kukua ,” alisema.
JAMII ZA FANGAS
Alibainisha kuwa, sumu hizo zina tabia tatu ambazo kusababisha kansa,
kupunguza uwezo wa kuku kujikinga na maradhi ya kuambukizwa na
kusababisha kuzaa viumbe wa ajabu.
Magoma alitaja fangasi hao kuwa ni aspegilus wenye sumu ijulikanayo
kitaalamu kama aflatoxins b1 inayopatikana kwenye mahindi, mashudu,
karanga na dagaa.
Aina nyingine ya fangasi ni ‘penicillium’ ambao wana sumu iitwayo
ochratoxin A. Japo fangas hawa wanatengeneza dawa kama peniciline au
PPF ambayo hutibu maradhi mengi wana sumu wanapotumiwa kwa utaratibu
huo.
Fangasi wengine kwa mujibu wa Magoma ni fussanum wenye sumu ya
fumonisins T-2 hawa ni jamii ya fangas wanaoonekana kwenye nafaka
zikiwamo mahindi mchele na mtama.
UAMBUKIZAJI SARATANI
“ Kuku akila sumu hizi hupata kansa, kwa hiyo mwanadamu anaambukizwa
kutokana na mabaki ya sumu hizo zilizo kwenye mwili wa kitoweo hicho na
ataupata ugonjwa atakapokula mara nyingi nyama ya kukua” alionya.
Magoma alisema sumu hizo hupatikana katika mazingira ya uzalishaji kama
joto, unyevunyevu unaoonekana kwenye mazao kuanzia utayarishaji
mashambani hadi matumizi majumbani.
Aidha, kutokana na ukubwa wa tatizo mtaalam huyo aliwashauri wafugaji
kutumia dawa ya mycotoxin binder au check-o-tox inayokamata sumu na
kuitoa kupitia njia ya choo.
Alisema moja ya kazi ya kirutubisho hicho ni kudhibiti sumu hiyo,
kupunguza unyevu kwenye chakula na huikusanya sumu kwenye mwili wa kuku
kisha kuitoa kwa njia ya haja.
Pia aliwashauri wafugaji kununua vyakula vya kuku kwenye kampuni
zinazozalisha kwa viwango na wale wanaotengeneza wahakikishe wanaweka
kirutubisho hicho ili kukabiliana na tatizo la kansa ya kuku.
Magoma alitaja dalili za ugonjwa huo kwa kuku kuwa ni mifuu yao kuwa na
madoadoa ya njano, ini lake kuwa kubwa zaidi na huwa na uvimbe kwenye
utumbo.
MFUGAJI AZUNGUMZA
Mfugaji wa kuku mkazi wa jijini Dar es Salaam, Jonesia John alisema
kutoka aanze ufugaji kuku wake wamekuwa wakisumbuliwa na mafua ambayo
yamekuwa yakiwasababishia kuwepo kwa idadi kubwa ya kifo.
Alisema ugonjwa mwingine ambao umekuwa ukiwasumbua kuku wake ni homa ya tumbo.
Kuhusu kansa ya kuku, alisema amekuwa akisikia wafugaji wenzake wakilalamikia hilo lakini hajawahi kushuhudia kuku mwenye nao.
Hata hivyo, alipoulizwa kama ana elimu yoyote ya ugonjwa huo ili pindi
mifugo yake itakapopata aweze kukabiliana nao, alisema mara nyingi
amekuwa akinunua vyakula salama vya kuku kwenye kampuni.
Pia alisema amekuwa akihakikisha mabanda na maeneo ambayo kuku wanakula yanakuwa safi wakati wote. SOURCE:
NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / UTAFITI: ULAJI WA KUKU WA KISASA (BROILA) CHANZO KIKUBWA CHA ONGEZEKO MARADHI YA SARATANI TANZANIA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment