BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU AKERWA NA WATU WANAOWAFUNDISHA WANAFUNZI KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA.

Minister of State in the Prime’s Office, Coordination, Policy and Parliamentary Affairs, Mr William LukuviMbeya. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi, amewataka wanafunzi nchini kuwa makini na ulaji wa mikate na pipi au vinywaji mbalimbali kwani upo uwezekano wa kuwekewa dawa za kulevya.

Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani, Iringa, alitoa rai hiyo juzi wakati akizungumza machache wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal kwenye maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya duniani ambayo kitaifa yalifanyikia mkoani Mbeya.
Alisema wapo watu wenye nia mbaya kwa wanafunzi na wanabuni mbinu ya kuwawekea kidogo kidogo dawa za kulevya kwenye mikate na pipi, vitumbua, maandazi na kwenye vinywaji kama vile juisi kwa lengo la kuwazoesha na matumizi ya dawa hizo.
“Kuweni waangalifu na mikate na pipi, soda na juisi mnazoletewa shuleni kwenu, kwani kuna watu wenye lengo la kuwazoesha kutumia dawa za kulevya kwa kuwawekea kidogokidogo,” alisema Lukuvi .
Lukuvi pia alisema wako vijana 403 wanaoshikiliwa nje ya nchi kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya na kwamba hakuna uwezekano kwao kurejea nchini kwani watahukumiwa kwa mujibu wa sheria za nchi hizo.
‘’Hawa vijana watahukumiwa kufungwa maisha na wengine watahukumiwa kunyongwa tu hawatarudi, hivyo ni lazima vijana mkaacha kutumika na vigogo na katika biashara hii’’,alisema.
Awali, Makamu wa Rais akihutubia alisema Serikali imewavalia njuga watu wanaojihusisha na usambazaji wa dawa za kulevya na kwamba inachohitaji ni wananchi kutoa taarifa.
Dk Bilal alisema tangu 2009 hadi sasa watu 13,846 wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya na kwamba tani 212 za bangi nazo zilikamatwa, huku kilo 969 za heroini zilikamatwa na cocaine kilo 363.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: