ARGENTINA NA UHOLANZI ZATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014.
Siku ya pili ya hatua ya nane bora ya michuano ya kombe la dunia imeanza kwa mchezo uliozikutanisha Argentina vs Belgium.
Mchezo huo umemalizika ubao wa matokeo ukionyesha ushindi wa 1-0 kwa Argentina, bao la mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain likiipeleka timu hiyo ya Amerika ya kusini kwenye nusu fainali.
Argentina itachuana na Uholanzi katika mchezo wa nusu fainali.
Uholanzi ililazimika kusubiri hadi kutinga nusu fainali mpaka hatua ya mikwaju ya penati katika mashindano ya kombe la dunia dhidi ya Costa Rica ikafanikiwa kushinda kwa penati 4-2.
Pia hii ni mara ya kwanza kwa Uholanzi kushinda mechi yoyote ambayo imevuka kwenda kwenye hatua ya dakika za nyongeza.
0 comments:
Post a Comment