BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKARI WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA NDEGE NCHINI KENYA, NI MUDA MCHACHE BAADA YA KUPAA NA KUANGUKA ARDHINI.


Ndege yenye namba ya usajili
5Y-CET iliyokua ikitokea uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi, Kenya kuelekea Mogadishu, Somalia ilipoteza mwelekeo na kuanguka katika eneo la Utawala dakika chache baada ya kupaa.
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya Julai 02 na inaaminika kwamba ndege hiyo ilikua iondoke mapema kusafirisha zao la Mirungi na bidhaa nyingine kuelekea Somalia.

Walinzi wawili wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambapo mmoja amekwishapatiwa matibatibu na kuruhusiwa huku mmoja akiwa bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Mama Lucy.

Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi Jijini Nairobi Benson kibue, ajali hiyo imetokea baada ya Ndege hiyo kuanguka juu ya Paa la jengo la kibiashara wakati ikijaribu kutua ghafla na kushika moto papo hapo.

Polisi wanaendelea na uchunguzi kufuatia ajali hiyo ndani ya mabaki ya ndege.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: