BINTI WA 16 ACHINJWA KAMA KUKU MANYONI MKOANI SINGIDA, HOFU YATANDA.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela
WATU wasiojulikana wilayani Manyoni wamemchinja mithili ya kuku binti mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 16.
Diwani wa Kata ya Manyoni Mjini, Hamis Masabuni alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi katika eneo la Mitoo kwenye mashamba ya Magereza, Uwanja wa Ndege wa zamani.
Alisema siku ya tukio, yeye alipata taarifa ya simu kutoka kwa raia wema hivyo ikambidi aende huko kushuhudia kulikoni na mara alipofika eneo hilo alikuta mwili wa marehemu ukiwa umelala chini na kuchinjwa mithili ya kuku.
Diwani huyo amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili kubaini wauaji wa binti huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni, Getruda Njughuda amekiri kuupokea mwili wa binti huyo.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.HABARILEO.
0 comments:
Post a Comment