Umoja wa Mataifa umesema robo
tatu ya Wapalestina waliouawa kwa mashambulizi ya ndege yanayoendelea
yanayofanywa na Israel huko Gaza ni raia wa kawaida.
Maafisa wa Palestina wanasema raia mia moja ishirini wameuwawa tangu mashambulio kuanza.
Professor Manuel Hassassian mwakilishi wa Palestina nchini Uingereza, ameiambia BBC, Israel kwa kuwalenga Hamas hukutakwepa kuwadhuru raia.
Alisema idadi kubwa ya raia wamekufa siyo sababu Hamas inajificha kati ya raia, yaani inawatumia raia kama kinga.
Gaza, kwa hivo wanapowalenga Hamas kamawanavosema, wanawalenga wa-Palestina wote. Siyo Gaza peke yake.Katika Ufukwe wa Magharibi piya, Israil imekuwa ikiwauwa kiholela, na huko hakuna makombora yaliyolegwa dhidi ya Israil" Alisema Hassassian. BBC.
0 comments:
Post a Comment