BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JIJI LA ARUSHA SIYO SALAMA TENA, MILIPUKO KILA KUKICHA, HII YATOKEA KATIKA MGAHAWA.


Hali ya usalama imezidi kuwa tete katika Jiji la Arusha kufuatia mfululizo wa matukio ya raia kujeruhiwa kwa kinachoaminiwa kuwa mabomu ya kurusha kwa mkono baada ya jana usiku kutokea mlipuka katika mgahawa wa Kihindi ujulikanao kama Vama Restautant uliopo maeneo ya Gymkhana.



Taarifa zinaeleza kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa huku wawili wakielezwa kuwa katika hali mbaya sana.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi wakishirikiana na Askari Jeshi wamekuwa na kazi ngumu ya kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kilichotegwa nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo.

Ni wakati sasa wa vyombo vya usalama kuwa imara na kazi yao. Matukio haya ni mageni mno kwa utamaduni wa Watanzania.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: