BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBIO ZA URAFANSA NA COLOMBIA ZAISHIA MIKONONI MWA BRAZIL NA UJERUMAN KATIKA HATUA YA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA 2014 NCHINI BRAZIL.



Hatimaye hatua ya 8 bora ya michuano ya kombe la dunia imeanza jana usiku kwa michezo miwili kati ya wenyeji Brazil na Colombia huku Ufaransa dhidi ya Ujerumani.

Kwenye mchezo wa kwanza Ujerumani ilifanikiwa kuifunga Ufaransa 1-0 kwenye mchezo mkali uliozikutanisha timu hizo, goli la beki wa Borrusia Dortmund Matt Hummels alilofunga kwa kichwa katika kipindi cha kwanza likaipeleka Ujerumani nusu fainali ya tatu mfululizo tangu mwaka 2006.



Mchezo wa pili ulizikutanisha Brazil ambao ni wenyeji dhidi ya majirani zao Colombia.



Magoli ya mabeki Thiago Silva na Rafiki yake wa tangu utotoni David Luiz yakaipeleka Brazil kwenye nusu fainali dhidi ya Ujerumani.



Colombia walipata goli lao la kufutia machozi kupitia mkwaju wa penati wa mshambuliaji James Rodriguez, moaka refa anamaliza mpira Brazil 2-1 Colombia.



Katika mechi ya leo itazikutanisha Belgium Vs Argentina saa 1 usiku wakati Costa Rica vs Holland mchezo utaochezwa majira ya saa saa 5 usiku.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: