TASWIRA YA UGONJWA WA EBOLA AFRIKA, SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) LATANGAZA DHARURA.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka "hatua za dharura" zichukuliwe ili kudhibiti kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Africa magharibi, ambao umewauwa zaidi ya watu 400. Ugonjwa huu ndio mkubwa zaidi duniani kuzuka kutokana na visa vyake, vifo na kusambaa katika maeneo.
Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres (MSF) tayari limeonya kuwa kusambaa kwa ebola hakuwezi kudhibitiwa. Shirika hilo lina wafanyikazi 300 wa kimataifa na vile vile wa kitaifa wanaofanya kazi nchini Guinea, Sierra Leone pamoja na Liberia, ambako ugonjwa huo unaenea kwa kasi. Mataifa mengine yako macho iwapo ugonjwa huo utasambaa Zaidi.Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na ambao dalili zake za mwanzo huweza kuwa kushikwa na homa, kuwa dhaifu, kuumwa na misuli na kuumwa na koo. Na huo ni mwanzo tu: kile kinachofuata ni kutapika, kuendesha na -wakati mwingine- kuvuja damu.Virusi hivyo huenea kwa haraka sana, na hadi sasa hakuna dawa inayotambulika kuweza kuvitibu, kwa hivyo wanaotoa huduma za matibabu huvalia mavazi yanayowakinga kutokana na kuambukizwa kwa ugonjwa huo. Kulingana na uzito wa athari za ugonjwa huo, hadi kufikia asilimia 90 ya walioambukizwa huaga dunia. Anayehakikisha usafi anawakaribia wagonjwa wanaosubiri matokeo baada ya kupimwa damu.Vipimo vya maabara vitaonyesha kwa saa kadhaa iwapo sampuli ya damu inayopimwa ina virusi vya Ebola au la.Baada ya kukumbana na virusi hivyo katika sehemu iliyotengwa, mavazi na viatu husafishwa kwa Chlorine.PICHA/BBC
0 comments:
Post a Comment