BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UJANJA NA MBINU CHAFU ZAANZA MBIO ZA UCHAGUZI MOSHI, CHADEMA YACHEZEWA RAFU KALI.

http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/07/chadema2.jpg
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Moshi Mjini kimedai kuwepo kwa njama za kuingizwa kwa watu katika uchaguzi wa viongozi wa wilaya hiyo, ambao baadaye watatumika kwa maslahi ya vyama vingine vya siasa.

Hofu hiyo imekuja wakati CHADEMA Manispaa ya Moshi, leo inafanya uchaguzi wa kupata viongozi wapya watakaoiongoza kwa miaka mitano ijayo kwa mujibu wa katiba.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Jafary Michael alisema bado ni vigumu kuwabaini watu hao, kutokana na kwamba sifa za mgombea lazima awe mwanachama wa CHADEMA.

“Mpaka sasa hatuna tatizo, ingawa ni kweli kuna hofu hiyo, kwamba kuna nia ya kuingiza watu ambao wanaweza siku za baadaye wakafanya kazi kwa maslahi ya watu na vyama vingine vya siasa,” alisema Michael.

Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, wameamua kufuata katiba ili kuhakikisha kila mgombea anakuwa ni mwanachama halali na wanaamini kuwa kila atakayechaguliwa atakuwa na sifa stahiki za kuchaguliwa.

Michael ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, alisema kwa sasa Kamati ya Udahili inafanya kazi ya kupitia majina ya watu waliojitokeza kugombea ili kujiridhisha na sifa ambazo mgombea atapaswa kuwa nazo.

Alisema hadi jana jioni makada wa chama hicho walikuwa wamerejesha fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali, huku nafasi ya mwenyekiti akijitokeza mgombea mmoja tu.

Uchaguzi huo utafanyika katika Hoteli ya New Castle kuanzia saa 3 asubuhi.TANZANIA DAIMA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: