BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAUME WA KENYA AMCHANGANYA BINTI WA KIHINDI KATIKA MAPENZI, MUME ALIKUWA MFANYAKAZI KATIKA NYUMBA YA FAMILIA YA MWANAMKE, MAMBO YA UPENDO YALIANZIA HAPO !!!.


http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/08/07/140807110224_bukusu_darling__976x549_bbc_nocredit.jpgKumekuwa na msisimko mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Kenya kuhusu taarifa ya msichana wa Kihindi aliyekiuka mila na tamaduni za jamii yake na kuolewa na kijana Mwafrika.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/08/07/140807105812_bukusu_darling__976x549_bbc_nocredit.jpgMsichana huyu wa kihindi anaitwa Sarika Patel, na ameolewa na kijana wa kabila la Bukusu Timothy Khamala, jambo ambalo ni nadra sana kwa watu wa jamii ya kihindi. Kilichowashangaza wengi ni kwamba Sarika ametoka katika familia tajiri na kuamua kuishi maisha ya walalahoi kijijinihttp://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/08/07/140807105306_bukusu_darling__976x549_bbc_nocredit.jpgKwa Sarika maisha ya umaskini ambayo Timothy anaishi sio kikwazo hata kidogo bali kwake hapo ndipo anapata raha na mapenzi ambayo anasema yamemridhisha na kumtuliza nyumbani kwa kijana Timothy.http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/08/07/140807105220_bukusu_darling__976x549_bbc_nocredit.jpgTimothy alikuwa anafanya kazi nyumbani kwa kina Sarika kama mjakazi lakini akafutwa kazi na baba ya Sarika baada ya kupendana na msichana wake.Kwa sasa yeye ni tarishi katika ofisi hii ya jimbo.Sarika hana kazi http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/08/07/140807105353_bukusu_darling__976x549_bbc_nocredit.jpgWawili hao sasa wapo katika pilka pilka za kuanza maisha mapya ila kwa pingamizi kali . Sarika Patel anasema kulingana na mila yao si sawa kuolewa na mtu asiyekubaliwa au kuchaguliwa na wawazi wako. Wachumba kwa kawaida hutoka jamii sawa. http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/08/07/140807105521_bukusu_darling__976x549_bbc_nocredit.jpgMbali na tofauti ya rangi zao za ngozi , Sarika anatoka katika familia tajiri kinyume na mumewe Timothy ambaye ni mlalahoi. Licha ya tofauti hiyo, Sarika anasema wazazi wake hawangeweza kumzuia kumpenda amtakaye.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: