BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHEZEA EBOLA ! UGONJWA HATARI WA EBOLA WASABABISHA SERIKALI YA SIERRA LEONE ITOE AMRI YA WANANCHI KUJIFUNGIA NDANI ZA NYUMBA ZAO KWA MASAA 72.

Serikali inasema ikiwa juhudi z akupambana na Ebola zitashuka, madhara yatakuwa makubwa zaidi.

Rais wa Sierra Leone amesema kuwa serikali inatafakari kutangaza awamu ya pili ya amri ya kutotoka nje kote nchini ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa hatari wa Ebola.

Rais Ernest Bai Koroma, amesema kuwa kwa sasa ameridhika na mafanikio yaliyotokana na kuwazuia watu kutoka nje kwa saa 72.

Awamu ya kwanza ya amri hiyo ilimalizika Jumapili.
Alisema kuwa maafisa wakuu walizuru zaidi ya nyumba milioni moja na kuwapata watu wengi ambao walikuwa wameathiriwa na ugonjwa huo.

Pia walipata mili ya watu waliokuwa wamefariki kutokana na ugonjwa huo.

Shirika la afya duniani limesema kuwa hadi pale hatua zaidi zitakapochukuliwa kukabiliana na janga la Ebola, visa vya maambukizi huenda vikaongezeka.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: