MAKAMPUNI 130 YA CHINA YALAUMIWA KWA KUTENGENEZA VIFAA VYA MATESO NA KUSAMBAZA KWA JESHI LA POLISI DUNIANI.
Makampuni nchini China yameingia katika shutuma kali kuwa wanatengeza na kusafirisha vifaa vya mateso kwa vikosi vya polisi duniani.
Vifaa vya mateso.
Shirika la kutetea haki za binaadamu Amnesty International limetoa taarifa kuwa makampuni yapatayo mia moja na thelathini nchini humo,kati yao wamekiri kutengeneza vifaa hivyo ikiwemo vibanio vya umeme,viti vya umeme,na pingu za vidole gumba.
Inasemekana vifaa vingi japo hutengenezwa na kusafirishwa,vingi matumizi yake ni katika kuleta maumivu mwilini na mateso.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu lina shaka na nchi zenye ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu hasa Africa na Kusini Mashariki mwa Asia wao ndio wateja wakuu wa vifaa hivyo.BBC
0 comments:
Post a Comment