Na Mtanda Blog, Morogoro.
Mashindano ya Copa Coca Cola 2014 chini ya umri wa miaka 15 yameanza kutimua vumbi katika uwanja wa Sabasaba kwa kushirikisha jumla ya timu tano ambayo yatatoa nafasi kwa makocha kuteua wachezaji wataounda kikosi cha umri huo kwa ajili ya kuwakirisha mkoa wa Morogoro katika mashindano hayo ngazi ya taifa hapo baadaye.
Katibu mkuu mtendaji wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka alieleza kuwa hapa kuwa mashindano ya copa coca cola 2014 chini ya umri wa miaka 15 yanaanza kutimu vumbi leo Septemba 17 katika uwanja wa Sabasaba ikishirikisha timu tano.
Semka alitaja timu hizo kuwa ni pamoja na Morogoro Vijijini, Manispaa, Mvomero, Kilosa na Kilombero huku Ulanga ikishindwa kuleta timu kutokana na sababu mbalimbali za kiuongozi.
“Copa coca cola 2014 chini ya umri wa miaka 15 yanaanza kuchezwa leo katika uwanja wa Sabasaba kuanzia saa 3 asubuhi na saa 10 jioni na haya mashindano safari hii yanashirikisha timu za wilaya tano tu, kwanzi ndizo zilizothibitisha kuleta timu isipokuwa Ulanga wameshindwa kuleta timu pamoja na Gairo.”alisema Semka.
Semka alisema kuwa michezo hiyo inafanyika kwa siku mbili ambapo kila siku kutakuwa na michezo mitano na katika siku hizo jopo la walimu watakuwa na kazi ya kuteua wachezaji wa kuunda kikosi kitakacho wakilisha mkoa wa Morogoro katika mashindano ya copa coca cola ngazi ya taifa.
0 comments:
Post a Comment