BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UZEMBE WASABABISHA TIMU YA SOKA U23 YA TANZANIA KUSHINDWA KUSHIRIKI MICHEZO YA OLIMPIKI 2016.

 
Dar es Salaam. Tanzania haitashiriki michezo ya soka kimataifa hadi mwaka 2016 kutokana na timu yake ya vijana wa umri chini ya miaka 23 kutoshiriki michuano ya kusaka tiketi ya kushiriki Olimpiki msimu wa 2015/2016.


Kukosekana kwa timu hiyo ya U-23 kunaweza kuwa uzembe wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Katika ratiba iliyotolewa juzi na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), pazia la michuano hiyo litafunguliwa Desemba.


Katika michuano hiyo, raundi ya kwanza Rwanda itaanza kukata utepe kwa kumenyana na Somalia wakati Kenya itacheza na Zambia au Botswana.


Kikosi hicho mara ya mwisho kilishiriki michezo ya Afrika mwaka 2011, kikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kiliondolewa mapema kwenye michuano hiyo na Nigeria.


Hata hivyo, U-23 haitashiriki michuano hiyo kwa vile Tanzania haikuthibitisha ushiriki wake huku viongozi wa juu wa TFF wakikwepa kulizungumzia suala hilo.


Alipoulizwa juu ya suala hilo Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kwa kifupi :”Sina taarifa nipe muda nifuatilie.”


Kwa upande wake, Julio akizungumzia suala hilo alishutumu TFF kwa uzembe kwa kushindwa kufatilia wakati Tanzania mara ya mwisho ilifanya vizuri ingawa ilitolewa hatua za mwisho.


“Kilichopo ni uzembe tu wa wahusika wameshindwa kufuatilia.” Timu hiyo ya U23 ndiyo chimbuko la kina Shomari Kapombe, Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu na nyota wengine.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: