BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARA WALIOKUWA WAKIPEANA MAHABA WAKIWA NA SARE ZA JESHI LA POLISI, WATIMULIWA KAZI.


Kamanda a Polisi Mkoani Kagera Henery Mwaibambe ameeleza waandishi wa habari muda mfupi uliopita kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi.

Kwamba walikuwa wanafanya kazi katika Wilaya ya Misenyi.


Polisi Mkoani Kagera imewafukuza kazi Askari wake watatu kwa kuweka picha za mahaba kwenye mitandao ya kijamii. 

Askari hao walikuwa wanafanya kazi kikosi cha usalama barabarani Wilayani Missenye.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Henry Mwaibambe amesema picha hiyo sio ya kuchakachua na ilipigwa na askari mwenzao ambaye pia amefukuzwa kwa kuwa kitendo hicho kimelidhalilisha jeshi la Polisi.


CHANZO:http://www.jamiiforums.com
"Askari wa usalama barabarani waliopiga picha ya mahaba wakiwa na sare za Polisi wafukuzwa kazi"
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: